Thursday, November 1, 2012

WAKAZI WA DAR WAFURAHIA USAFIRI WA GARI MOSHI


Bi. Rose Ngauga akizungumza na mwandishi wetu aliyemtembea ofisini kwake kujua mawili matatu kuhusiana na usafiri huo. WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wamefurahia kuanza kwa usafiri wa treni waliousubiri kwa muda mrefu ulioanza juzi.

Abiria wakigombea kupanda treni kutoka katikati ya jiji kueleke Ubungo.
Kamera yetu leo ilitua katika ofisi ya mkuu wa kituo kinachodili na usafiri huo, Bi. Rose Ngauga na kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na usafiri huo.
Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.

Wanafunzi wakipanda katika behewa lao maalumu tayari kwa safari.

Bi. Rose akimuonyesha mwandishi wetu (hayupo pichani) tiketi zinazotumika kwa abiria wa kawaida na wanafunzi.

Abiria wakiwa katika dirisha la kukatia tiketi.

Wanafunzi wakikata tiketi katika dirisha maalumu kwa ajili yao.


Kichwa cha treni kikiunganishwa na mabehewa kabla ya kuanza safari.
Abiria wakiwa wameketi ndani ya behewa wakisubiri kuanza safari.
Mkuu wa Kituo cha Reli, Bi. Rose Ngauga akikagua mabehewa kabla ya gari moshi kuanza safari leo saa 9.40 alasiri.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...