Wednesday, October 17, 2012

WAREMBO WA REDDS MISS TANZANIA WALIPOTEMBELEA MAPANGO YA AMBONI TANGA



Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012, juzi walikamilisha zira yao ya Kutembelea Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga kujionea vivutio vya utalii katika mikoa hiyo ambapo walimalizia mkoani Tanga kwa kutmbelea Mapango ya Amboni mkuano humo.

Warembo hao wakiwa katika mapango hayo ya kale waliweza kujionea vitu mbalimbali ambavyo ni vya kipekee na vyakuvutia vilivyopo katika mapango hayo ya asili ya zama za kale.
Miongoni mwa vitu vilivyopo huko kwenye mapango hayo ni sanamu za aina mbalimbali za Bikira Maria, Maandiko ya Quran, Daraja, sanamu za jinsia ya kike na kiume, chui, na vitu vingine mbalimbali vya kuvutia

Bado pango hilo la Amboni linaendelea kukua. Na hapa warembo wakiangalia moja ya vitu vinavoota kila mwaka hasa wakati wa mvua.
Hapa huna budi kuinama na huko ndani waweza kuinuka bila kugusa juu.Wanapotokea.

Warembo wakiangalia moja ya vitu vya kuvutia na hapa waliangalia mchoro wa asili wa chui aliyelala baada ya kushiba.

Hakika ukifanikiwa kupita hapa utapita pango zimana kujionea vitu vingi. Hapa lazima utambae na wengi hushindwa kupenya hapa.
Ni full kushangaa kwa warembo hawa wa Redds Miss Tanzania 2012. Hakika ni utalii wa ndani uliofanywa na warembo hawa lakini je ni watanzania wangapi tunatalii katika maeneo ya utalii.
Wakionesho eneo ambalo linafananishwa na daraja kwa jinsi lilivyo umbika.

Hapa ni katika eneo ambalo linafananishwa na Mlima Kilimanjaro na hapa warembo wakipanda mlima huo ndani ya Mapango ya asya Amboni mkoani Tanga.
Wakionesho eneo ambalo linafananishwa na daraja kwa jinsi lilivyo umbika.

Hapa warembo wakipiga picha katika kiti cha enzi. Ni jiwe lililochongeka mithili ya sofa na ukiingia pangoni humo inapendeza kuchukua kumbukumbu

Eneo hili ni linafananishwa na Mlango wa kupandia ndege na hapa warembo wakipanda na kutoka nje ya pango

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...