Tuesday, April 3, 2012

WANAMITINDO WA BONGO WASHIRIKI ONESHO LA MAVAZI LA WIKI AFRIKA KUSINI


Baadhi ya wabunifu hao wakipita jukwaani  kuonyesha moja ya vazi lao.

 Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Rita (wa tatu kushoto), akiwa katika pozi na baadhi ya wabunifu wa mavazi hayo.
WABUNIFU wa mavazi watatu watanzania wanaoshiriki onesho la wiki ya mavazi Afrika Kusini wametia fola katika onesho hilo.

Wabunifu hao walishiriki onesho hilo kufuatia mwaliko wa mwanamitindo mahiri Millen Magese ambapo walionesha katika shoo iliyoitwa Tanzania International Fashion Exposition (TIFEX).

Wahudhuriaji waliofika kuona shoo ya watanzania hao walikuwa wengi na walivutiwa zaidi na namna ambavyo walichanganya kitenge katika kupendezesha mavazi yao.

Mbunifu Evelyn Rugemalila ndie alifungua pazia kwa kuonesha mavazi yake aliyoyanakshi kwa kanga, aliweza kuzikonga nyoyo za washabiki na kujikuta wakimpigia makofi mara alipomaliza shoo yake.

Kitu ambacho alikifanya tofauti na wabunifu wengine ni wakati anamalizia shoo yake alitembea jukwaani akiwa amewavalisha sare ya nguo za kanga iliyofanana na yake huku.

Baada ya Evelyin kuonesha ilifika zamu ya mbunifu wa mavazi Jamila Swai kuonesha mavazi yake ambapo aliongozana na mbunifu wa mikoba kutoka mradi wa Fahari wa Zanzibar Julie Lawrence.

Wanamitindo wa kizungu na kiafrika wakiongozwa na mwanamitindo mahiri nchini Millen Magese waliwakilisha vema ambapo kila alipokuwa akitokea Millen watu walishangilia.

Baada ya Jamila alifuata Doreen Noni aliwakilisha lebo yake ya Eskado Bird alifuata ambapo naye alitumia viashiria vya kanga pamoja na ngozi ngozi katika nguo zake.

Kwa pamoja wabunifu wa Tanzania walifanya vema katika onesho hilo huku wanamitindo nao wakiwa wamejitaidi kuonesha umahiri katika kutembea.



Mwanamitindo huyo akikatiza jukwaani.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...