Monday, April 2, 2012

WAFANYAKAZI WA AIRTEL NA WATEJA WAO WAJUMUIKA QUALITY CENTRE DAR

Watoto wa wateja na wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wapatao 150 wakiwa pamoja wakiwa katika shamra maalum ya watoto kuelekea sikukuu ya Pasaka ambapo Jumamosi iliyopita (juzi) walijiburudisha kwa michezo mbalimbali iliyofanyika kituo cha michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport ndani ya jengo la Quality Center Jijini Dar-es-Salaam Barabara ya Nyerere
Meneja Mauzo wa Airtel Tanzania, Bi.Hilda Nakajumo, akikata keki kwa ajili ya watoto hao.

Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania, Bw.Irene Madeje, akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe hiyo.

Huu ni mkakati ambao Airtel imejiwekea kusherehekea pamoja na watoto wa wateja wao wa makapuni ( corporate customer) wiki moja kabla ya sikukuu za Pasaka lengo likiwa ni kuwa karibu na wateja wao na
kusambaza upendo wa kampuni hiyo kwa wateja wake na familia zao.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Bi Irene Madege alisema: "Leo tunajisikia furaha kuwa na watoto wa wateja wetu na kujumuika nao pamoja, tumekuwa tukifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni katika kuwazawadia wateja wetu, lakini leo tunatumia muda huu kuwapa burudani watoto ambao ndio wateja wetu wa kesho".

Kwa muda wa takribani masaa manne, watoto zaidi ya 150 walipata burudani mbalimbali ikiwa pamoja na michezo mbalimbali ya watoto kama “face painting”, mashindano ya kucheza muziki, na pia kupata nafasi ya kukutana na wafanyakazi wa Airtel, kumzungumza pamoja na kuwasisitiza watoto kuwa wasikivu shuleni ili kufanya vizuri kwenye masomo yao.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...