Thursday, March 8, 2012

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI....

Upokeaji wa kitabu kwa ajili ya wanafunzi, The Dutches of Cornwall Camilla
Parker Bowles (kushoto)akikabidhi kitabu kwa Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete kwenye viwanja vya WAMA jijini Dar es Salaam (kulia) kitabu hicho ambacho kimetimiza idadi ya vitabu milioni moja vilivyotolewa na kutoka kwa taasisi ya British Charity READ International. (2012).

 
Katika maadhimisho hayo ni vyema kujikumbusha matukio ya picha za matukio ya kazi mbalimbali zilizofanywa na Mke wa Rais ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, katika mchango wake wakumkwamua kimaisha mwanamke wa Tanzania pamoja na kusaidia kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ni mfano wa kuigwa na baadhi ya wake wa viongozi wengine kwa kuuonyesha mfano wa upendo katika jitihada za kuwakomboa wanawake wenzake kutoka katika dimbwi la umaskini na kuwasaidia mitaji na vifaa mbalimbali ikiwapo uanzishwaji wa vikundi kupitia taasisi yake ya WAMA,Ili kujikwamua kimaisha nchini Tanzania.Katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani, Kupitia habari picha utamfahamu Mama Salma Kikwete ujasiri wake katika kumletea maendeleo mwanamke pamoja na watoto wa Kitanzania.

 
Kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  akijadiliana na wanafunzi wenye vipaji maaluum katika maabara ya chuo hicho jinsi ya upasuaji wa mnyama .Mama Kikwete alitembelea Malaysia 2011.
 
Picha ya chini, wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki matembezi ya kuchangia watoto jijini Dar es Salaam 2011, (kulia) ni Picha ya kushoto, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki matembezi ya kuchangia watoto jijini Dar es Salaam 2011, (kulia) ni Mkurugenzi wa Benki ya Barcklays Kihara Maina.

Mkee wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha watoto jinsi ya kunawa mikono salama na sabuni wakati wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam 2011.


ANGALIZO
Kuna matukio mengi ya maendeleo yanaoyofanywa na Taasisi yake kaatika kusaidia jamii. Haya ni machache katika mwaka jana lakini kutokana na nafasi pokea haya, natumaini utafurahia ubunifu wangu kama mdau wako mwanamke kukutayarishia kama mchango wangu mdogo katika kuadhimisha siku ya WANAWAKE DUNIANI,

Nawatakia sikukuu njema – Wanawake lazima tusimame imara daima tusikubali kunyanyaswa, tujitambue na kujiamini.

Imetayarishwa na Mdau Mwanakombo Jumaa
Picha/Habari: sufianimafoto blog

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...