Friday, March 9, 2012

MAZOEZI YA  CHEZA, VAA, IMBA KAMA RIHANA PATASHIKA NGUO KUCHANIKA


Babro Beckerham akijibidiisha mazoezini hapo.

WASHIRIKI wa Shindano la Cheza, Vaa, Imba kama Rihanna, wamezidi kujipa kashikashi katika mazoezi ya kuhakikisha kila mmoja wao anaondoka na kitita cha shilingi milioni 10 wanazoshindania.

Washiriki hao nane waliobaki katika shindano hilo wanafanya mazoezi ya kufa na kupona kwaajili ya kuvaana kwenye nusu fainali inayotarajiwa kufanyika jumapili hii ndani ya Kiwanja cha Burudani cha Dar Live kilichopo Mbagala Zakheem jijini Dar es Salaam.

Washiriki hao watakuwa wa kwanza kutumbuiza jukwaani hapo kabla ya burudani za Mnanda, mduala kuanza kurindima usiku huo.

Mmoja wa washiriki wa shindano hilo Rukia Mohamed (katikati), akijifua namna ya kucheza na madensa wake wakati wa michuano hiyo.

Wellu Sengo (katikati), akijaribu kutumia madensa hao kwenye mazoezi tayari kwa mpambano wa jumapili.

Zalha Sadallah akijifua kwa bidii na madensa hao.

Mshiriki wa shindano hilo Like Abraham, akijifua kwa hisia kali.


Aisha Hassan akijikomaza namna ya kuuimba na kucheza staili za Rihanna.

Anatolia Raphael (katikati), akijinoa namna ya kutumia jukwaa siku hiyo.

Washiriki hao wakijifua kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...