LILIAN INTERNET, ALLY AKIDA KUTAMBULISHWA NYUMBANI LOUNGE
SHOO maalum ya utambulisho wa wasanii wapya waliojiunga na bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa, inatarajiwa kufanyika KESHO katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, ambapo mnenguaji Lilian Tungaraza ‘Liliani Internet’ na Mchalaza Gitaa Ally Akida
waliowahi kupiga mzigo ndani ya bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta Internatinal,’ walijunga na Mashujaa wiki iliyopita kwa kusaini mkataba wa kuitumikia bendi hiyo kwa muda wa miaka miwili.
Mbali ya Mashujaa , onyesho hilo pia litapambwa na Machozi Band inayomilikiwa na Mwanadada Lady Jay Dee ambapo kutakuwa na mambo mazuri ya kuvutia.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa viongozi wa bendi hiyo Luhanga alisema kuwa, “Si onyesho la kukosa kwa mpenda muziki wa dansi kwani pamoja na utambulisho wa wasanii wetu wapya, bendi hizi zinatarajiwa kukonga kwa nyimbo zake kadhaa sambamba na shoo ya nguvu toka katika sdafu zao za unenguaji,”Alisema Luhanga.
Naye Lilian akizungumzia hatua ya kuhamia kwake Mashujaa alisema kilichompeleka huko ni maslahi mazuri mazuri anayolipwa kwa kazi yake sambamba na fedha ya kujikimu kwa masuala mbalimbali ikiwemo matibabu, usafiri na nyumba.
Alisema pamoja na hilo amekwenda huko kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi katika harakati zake hizo za kusaka maisha kupitia muziki huku akiwaahidi mambo makubwa mashabiki wa bendi hiyo na muziki wa dansi kwa ujumla.
Internet amekuwa msanii wa pili kunyakuliwa na Mashujaa Musica hivi karibuni toka Twanga Pepeta ambayo mapema mwaka huu ilimchukua mwimbaji Charles Gabriel ‘Charlz Baba’ kwa lengo la kuimarisha kundi lao.

No comments:
Post a Comment