Wednesday, March 7, 2012

AIRTEL YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA WAKE

 
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Ellangallor akiongeaa na
wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa programme ya Airtel service
Academy iliyofanyika leo katika Makao makuu ya Airtel Morocco
Airtel Tanzania yadhamiria kuboresha huduma kwa wateja

* Watoa huduma 99 kuongezewa ufanisi

* Katika siku 365
Airtel Tanzania, mtandao unaoongoza kwa gharama nafuu na wenye wigo
mkubwa Tanzania leo umezindua programu ya kuwawezesha wafanyakazi wake
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wateja wake wanapata
huduma bora Tanzania.
Hii inakuja baada ya ya uzinduzi mzuri wa chuo cha masoko
kilichozinduliwa mwezi wa kumi mwaka jana inayojulikana kama " Airtel
Centum Sales University (ACSU)"
Akiongea katika uzinduzi wa programu hii ya mafunzo kwa timu
zinazotoa huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel ,Mkurugenzi wa
Airtel Tanzania bwana Sam Elangalloor alisema,"Leo tunazindua rasmi
mafunzo ya huduma kwa wateja Tanzania inayoashiria dhamira yetu katika
kuleta mabadiliko na kuwaopa wateja wetu huduma bora na zenye viwango
vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.lengo letu ni
kuhakikisha tunatoa huduma ambazo zinazidi matarajio ya wateja wetu na
kudumisha mahusiano ya muda mrefu.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha huduma kwa uteja, Adriana Lyamba
aliongeza kwa kusema, " mafunzo haya ni muendelezo wa kuonyesha ni kwa
jinzi gani kampuni na nembo yetu inajali wateja wake.Katika siku 365
zijazo wafanyakazi wa Airtel katika kityengo cha huduma kwa wateja
watajifunza mbinu za kitabia na zile za kikazi katika kutoa ufanisi
zaidi na kuwaongezea ujuzi zaidi.
Leo Tanzania zaidi ya wafanyazi 99 wa kitengo cha huduma kwa wateja
wataanza mafunzo haya ya huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel
makao makuuIn
Programu hii ya Airtel service Academy inatolewa na kampuni ya
ukufunzi ijulikanayo kama Centum learning na itahakikisha watoa
huduma wa Airtel wanakua bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla


Wafanyakazi wa Airtel pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika
uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha
wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi
iliyofanyika katika Makao makuu ya Airtel Morocco.



Keki maalumu ya uzinduzi wa programme ya Airtel Service Academy

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...