Saturday, March 17, 2012

BONGO MOVIE WASHEHEREKEA MWAKA MMOJA WA CLUB YAO


WASWAHILI wanasema kuwa msanii ni kioo cha jamii anaweza kukufundisha, kukuchekesha na kukuudhi lakini kwa usiku wa kuamkia leo Machi 17 kipengele cha kuchekesha ndicho kilichukua nafasi katika sherehe ya kutimiza mwaka mmoja ya Klabu ya Bongo Movie kwani wote waliohudhuria hafla hiyo walitoka ukumbini wakiwa wameshikilia mbavu zao kutokana na vituko vilivyofanywa na wasanii.


Sherehe hiyo ya kutimiza mwaka mmoja ilichukuwa nafasi katika Ukumbi wa Business Park uliopo Victoria jijini Dar, ambapo Bendi ya Mashujaa Musica ilikuwa ikisindikiza sherehe hiyo.


Akizungumza na mtandao wa Global Publishers Mwenyekiti wa klabu hiyo, Jacob Steven ‘JB’ alisema kuwa amefarijika sana kuiongoza klabu hiyo hadi kufikia ilipo sasa.


“Unajua kuongoza watu ambao wanajua kila kitu au wanavipato vikubwa ni kazi ngumu sana lakini nashukuru hadi leo hii hakuna mwanachama yeyote aliyenivunjia heshima,” alisema JB.




Irene Uwoya (kulia), akifuatilia baadhi ya matukio yaliyokuwa yakiendelea mahali hapo na rafiki yake wa karibu Johari.




Mama Dotnata akibadilishana mawazo na mme wake na rafiki yao.



Baadhi ya viongozi wa Bongo Movie wakitumbuiza mahali hapo.



Msanii wa filamu Nora naye alikuwepo.


Jack Pentezel akiunda pozi mahali hapo
Steve Nyerere akimpa maelekezo Wema Sepetu wakati akiingia ndani ya ukumbi.

Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo ilifanyiwa ubunifu mkubwa kwani ilikuwa na umbo la kamera.

Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani akielekea jukwaani kwa ajili ya kuwasha mshumaa uliokuwa juu ya keki.

Ridhiwani akiwasha mshumaa.

Mwenyekiti wa Bongo Movie, JB akimlisha keki Ridhiwani.

Sikubali na wewe ngoja nikulishe.

Ray akijiandaa kufungua shampeini.

Single Mtambalike ‘Richie’ au Bonge la bwana akiwajibika jukwaani.

Siyo kuigiza tu hata nyonga najua kuzungusha, Mainda huyo.

Uwoya, Hartman Mbilinyi na Mama Rolaa wakiwa kwenye pozi la nguvu.




No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...