Monday, February 20, 2012

MADIWANI MBEYA WAUNGUZA  MAFUTA YA GARI  KWENDA MORO KUSHANGILIA MPIRA

Meya wa Jiji la Mbeya, Mh. Kapunga (aliyesimama) akiwaongoza madiwani wake kuishangilia timu yao.

Baadhi ya maofisa wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya waliofika Uwanja wa Jamhuri jana.

Baadhi ya magari ya serikali yaliyotumika katika msafara huo. Mbele ni Meya Kapunga wa Jiji la Mbeya.

Mh. Kapunga akiwa na wachezaji wa halmashauri yake.

Wachezaji na maofisa wa Mbeya katika picha ya pamoja.


WANANCHI mkoani Morogoro jana jioni waliwashutumu vikali madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kitendo chao cha kutumia magari manne ya serikali kutoka jijini Mbeya hadi Manispaa ya Morogoro kuja kuishanglia timu yao ya Mbeya City kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Small Kids ya Rukwa inayotumia Uwanja wa Jamhuri kama uwanja wake wa nyumba.

Mchezo huo hakuwa na umuhimu wowote kwa kuwa timu hiyo ya Mbeya kabla ya mchezo huo ilishapata nafasi ya kucheza hatua ya tisa bora.

Baada kuona msululu wa magari hayo ya madiwani yalioongozwa na meya wao, Athanas Kapunga na mkuu wa Wilaya wa Mbeya, Evans Balama, wananchi wachache waliokuwepo uwanjani hapo walishindwa kuvumilia na kuamua kuwazomea madiwani hao huku wakiwatupia maneno ya kejeli kwa kufuja fedha za wananchi ambapo yalitumika magari sita ya serikali kuwaleta Morogoro.

Haa hivyo, meya wa jiji hilo, Kapunga, ambapo alipotakiwa kujibu shutuma hizo alisema halmashauri ilikuwa na fungu la michezo na waliwajibika kuja kuwapa sapoti vijana wao, wakiongozwa na mkuu wao wa wilaya ma Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, James Jorojick.

Mchezo huo ulimalizika kwa ‘madiwani’ hao kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-0 ambapo kocha wao, Juma Mwambusi, alisema waliupa umuhimu pia kama michezo mingine.





No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...