Monday, February 20, 2012

KIDUM AMCHEZEA FAULO DOKII KWENYE FAMILY DAY BONANZA DAR LIVE

Msanii kutoka nchini Burundi, Jean Pierre ‘Kidum’, akikamua na mmoja wa wasanii wa Bongo, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’, aliyekuwa mshereheshaji wa bonanza hilo.
…Akicheza na mmoja wa mashabiki zake.

…Akimshikia maiki mmoja wa wapiga vyombo wake.

Mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Sunday Mangu ‘Linex’, akitumbuiza.
….Akikamua kwa hisia kali.
Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Omar Kopa, akiwajibika.

Kiongozi wa ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’, Hassan Bichuka, akiwaburudisha mashabiki wake.

Wanenguaji na baadhi ya waimbaji wa Sikinde wakionyesha uwezo wao jukwaani.
Mwanamuziki chipukizi, Alex Machejo, akikonga nyoyo za mashabiki.
...Akionyesha hazina yakeya usanii.
Baadhi ya ‘Kina Rihanna’ walioingia 12 Bora wakiwa katika pozi.
...Walivyowatoa udenda mashabiki.
...Baadhi yao wakiangua kilio baada ya kutolewa kwenye kinyang’anyiri hicho.
Wasanii wa ngoma za asili wa Machozi Bendi wakichenguliwa na jukwaa hilo.
Wanamuziki wa Mawazo Group wakionyesha staili yao.
Mcheza sarakasi wa Mawazo Group Band akionyesha ‘maajabu’.
Msanii akionyesha ukali wake.
Shabiki akilimaindi jukwaa alipopewa fursa ya kuonyesha machejo.
Baadhi ya watoto waliofika kituoni hapo wakijiburudisha kwa kuogelea.
Msanii mdogo mwenye ‘swagger’ za kiutu uzima, Hamisi Fadhili aka ‘Dogo Lila’, akiimba kwa mbwembwe.
...Akionyesha uwezo katika kucheza.
Sehemu ya umati uliofurika kituoni hapo.
MOTO mkali uliendelea kuwaka kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala jijini Dar usiku wa kuamkia leo ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo: Linex, Khadija Kopa, Alex Machejo, na makundi ya ngoma za asili ya Machozi na Mawazo Group, bendi ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’, Dogo Lila na msanii Kidum kutoka nchini Burundi, wote hao walikamua sambamba na washiriki wa shindano la ‘Cheza, Vaa, Imba Kama Rihanna’ na kuufanya umati mkubwa ulifoka hapo kupata burudani isiyopimika katika hali yoyote.

Wasanii hao walitumbuiza kwenye Family Day Bonanza ambalo hufanyika kila siku ya Jumapili chini ya usimamizi wa uongozi wa kituo hicho cha Dar Live kilichopo Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaam



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...