Sunday, January 24, 2016

YANGA YAICHAPA 3-0 FRIENDS RANGERS TAIFA

Washambuliaji wa timu ya Yanga SC, Paul Nonga na Simon Msuva wakiwa wamekumbatiana wakati wakishangilia bao lililofungwa na Msuva.
 TIMU ya Yanga SC, mapema leo imefanikiwa kutinga raundi ya 16 bora kwenye michuano ya ya Azam Sports Federation Cup maarufu kama FA baada ya kuichapa magoli 3-0 timu ya Friends Rangers ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga Paul Nonga akiwatoka mabeki wa timu ya Friends Rangers.
Msuva kushoto akionyesha uwezo wake uwanjani hapo.

Saturday, January 23, 2016

SIMBA YAIKUNG'UTA 3-0 BUKINAFASO YA MOROGORO

Mshabuliaji wa kimataifa wa timu ya Simba SC, Hamisi Kiiza (kulia), akipambana na mmoja wa wachezaji wa timu ya Bukinafaso ya mjini Morogoro katika mchezo wa FA uliyochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro. katika mchezo huo timu ya Simba imeibuka kidedea kwa kuichapa Bukinafaso magoli 3-0.
Mwinyi Kazimoto akimpongeza Saidi Ndemla, muda mfupi baada ya kuifungia timu hiyo goli la pili.
Wachezaji wa Simba SC. wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mehi hiyo kuanza katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Timu ya Bokinafaso ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo kuanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunga Zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli


Rais Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Monduli. (hawapo picha).
Rais Magufuli (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa ufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha jana.Rais Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medani.Rais Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.
Rais Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange.Rais Magufuli (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.Rais Magufuli akipewa maelezo ya zana mojawapo ya Kivita katika Zoezi la Onesha Uwezo Medani Mkoani Arusha. Picha na IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunga “Zoezi la Onesha Uwezo Medani” lililoandaliwa na kutekelezwa na Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu ambalo ni sehemu ya Jeshi la wananchi Tanzania katika eneo la Lang’arurusu nje kidogo ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.

Akizungumza na Askari na Maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania kabla ya kufunga zoezi hilo, Rais Magufuli amesema katika awamu yake ya tano ya uongozi amedhamiria kulitumia Jeshi la wananchi Tanzania katika kujenga uchumi, ikiwemo kuanzisha viwanda na kampuni za ujenzi ili kuharakisha maendeleo.

Ametoa mfano wa kiwanda cha Nyumbu ambacho kipo chini ya jeshi la wananchi Tanzania na kueleza kuwa wakati umefika wa kukiimarisha na kukiendeleza kiwanda hicho, ili kiweze kufanya uzalishaji mkubwa kwa manufaa ya nchi ikilinganishwa na hali ilivyo hivi sasa.

“Zipo nchi nyingi ambazo majeshi yao yanatumika katika uchumi na yanafanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano, wakati umefika na sisi kufanya hivyo. Hata hizi sare za jeshi na viatu, hatuna sababu ya kuvinunua kutoka nje ya nchi, tunaweza kutengeneza sisi wenyewe” Alisisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuandaa “Zoezi Onesha Uwezo Medani” ambalo limethibitisha uwezo, weledi na utayari lilionao katika jukumu lake la kiulinzi.

Ameahidi kuwa ataendeleza juhudi zilizofanywa na viongozi wenzake waliotangulia za kuliimarisha kwa vitendea kazi na maslai ya wanajeshi ili liweze kutekeleza wajibu wake bila vikwazo.

Pamoja na kuwapongeza Askari na maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania walioshiriki katika zoezi hilo, Rais Magufuli ameagiza Askari Mgambo na Askari wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) walioshiriki zoezi hilo kuajiriwa na jeshi la wananchi Tanzania.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Rais Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Wizara yake itaongeza na kusimamia juhudi za kuliboresha jeshi hilo kwa zana, vifaa na maslai kwa wanajeshi ili kuwajengea uwezo na morali ya kutekeleza majukumu yao ya kuilinda nchi, pamoja na kutoa msaada stahiki kwa nchi zenye kuhitaji ulinzi wa amani popote duniani.

Kwa upande wake Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Jeshi la wananchi Tanzania lipo imara na litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, nidhamu ya hali ya juu na uzalendo mkubwa.

Kabla ya kuwahutubia maafisa wa jeshi la wananchi, Askari na wananchi waliohudhuria ufungaji wa “Zoezi Onesha Uwezo Medani”, Rais Magufuli ameoneshwa zana mbalimbali za kivita ikiwa ni pamoja na kushuhudia upigaji wa mizinga ya masafa mafupi, masafa ya kati na masafa marefu.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha 
22 Januari, 2016

KIBA, JOKATE WATEMANA RASMI!

Staa wa Bongo, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’.


Dar es Salaam: Hii ni habari ya kipekee (Exclusive Story)! Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wanadaiwa kumwagana, Risasi Jumamosi ndilo gazeti pekee linaloweza kuthubutu kukupa mchapo kamili.

Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wakiwa katika pozi.

Habari ya mjini kwa sasa ni juu ya wawili hao ambao walikuwa gumzo kwa watoto wa mjini, kwa kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake tofauti na walivyokuwa awali huku chanzo cha kutengena kwao kikitajwa kuwa ni wazazi wa sehemu zote mbili kutoridhiana.


Ali  Kiba ‘King Kiba’.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, mbali na ishu ya wazazi, hivi karibuni Jokate na Kiba waliingia kwenye gogoro kubwa la kimapenzi baada ya kufumaniana kwenye simu, jambo ambalo limeendelea kutokea huku jamaa akiongoza kukutwa na meseji kwenye simu yake za mwanamke mmoja anayedaiwa kuishi nje ya Tanzania.

BOFYA HAPA KUSIKIA CHANZO
“Ukisema nikusimulie juu ya kumwagana kwa Jokate na Kiba basi tunaweza kukesha ila mbali na mambo ya wazazi, kwa kifupi tu ni kwamba, hawa watu wameingia kwenye mgogoro na kilichokuwa kikiwagombanisha mara nyingi ni uhusiano wao wa zamani.”

KIBA ANA DEMU?
“Mara kadhaa Jojo (Jokate) amekuwa akimlalamikia jamaa (Kiba) kuwa ana demu nje ya nchi ambaye amekuwa akimtundika katika mitandao ya jamii na kujinadi kuwa ndiye mkewe tofauti na wengi wanavyojua kuwa Jokate ndiye mtu wake.

“Mbali na hilo, sasa kuna suala la familia zao kuonesha hali ya kutokubaliana na wao kuoana hasa upande wa Jokate ambao ulionesha msimamo mkubwa kutomtaka hata kidogo Kiba, mambo hayo yamekuwa ni chagizo kubwa katika kuhatarisha mapenzi yao hivyo kufikia hatua hata ya wao kutoendelea kupendana kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo wa penzi lao.”

VIKAO VYAGONGA MWAMBA
“Tofauti na watu walivyozoea kuwaona pamoja, kwa sasa wametibuana na hapa tunapozungumza tayari kuna vikao kibao huko nyuma vilishakaa ili kunusuru penzi lao lakini imeshindikana maana kila mmoja sasa hivi anajifanyia mambo yake na hakuna dalili za kurudiana.

“Kiba anaonekana ameshajiingiza kwenye penzi la demu wake wa zamani huku Jokate naye akiwa ‘in love’ na mtu wake mwingine.”

MPANGO WA KUZAA WAYEYUKA
“Kitambo tu nimekuwa nikiwaambia kwa staili waliyokuwa nayo hakika wasingeoana hata kama ukiweka pembeni suala la dini zao kutoendana, maana kuna siku niliwasikia wakiambiana hata kama wazazi wakigoma wao wangefanya kila juhudi hata wazae pamoja tu.

“Lakini ukweli ni kwamba ilishindikana baada ya kuanza kugombana mara kwa mara, pamoja na kwamba Jokate alikuwa akikubalika kwa asilimia zote kwa mama Kiba na hata ndugu wengi wa Kiba walionekana kumpenda waziwazi,” kilisema chanzo hicho.

KIBA AFUNGUKA
Baada ya kupenyezewa mchongo huo, gazeti hili liliingia mzigoni kumtafuta Kiba ili atoe la moyoni juu ya madai hayo ya kumwagana na Jokate ambapo alipopatikana alisema kuwa haoni sababu ya kuzungumzia ishu hiyo kwani ni mambo binafsi.

“Kusema kweli ishu hii mimi sina uwezo wa kuiongelea zaidi kwa sasa kwani ni mambo binafsi sana na sioni faida ya kuzungumzia vitu ambavyo havina maana.
“Kwanza sioni nini cha kuongelea hapa kwani kila jambo lina mipaka yake,” alisema Kiba akikataa kuulizwa zaidi juu ya suala hilo.

JOKATE VIPI?
Kwa upande wa Jokate alipotafutwa kwa siku kadhaa ili azungumzie sakata hilo kwa ufasaha hakupokea simu ya mwandishi wetu hadi gazeti linaingia mitamboni.

PENZI LA JOKATE NA KIBA
Awali zilipovuja habari za penzi la Jokate na Kiba wote walikanusha, kadiri siku zilivyosonga ndivyo walivyozidi kuwa gumzo kwa mashabiki wao waliofurahishwa na ‘kapo’ yao huku wakionekana kwenye viwanja mbalimbali vya starehe wakiwa kimahaba lakini sasa mambo yanaonekana kwenda mrama.

OSTAZ JUMA: MIAKA 10 NA WANAMUZIKI ILITAKA KUNIVUNJIA NDOA YANGU!


Ostaz Juma Namusoma akiwa katika pozi.

UKIANZA kutaja majina ya mameneja mbalimbali wa muziki hapa Bongo, baadhi ya majina makubwa yasiyoisha miongoni mwao huwezi kulikosa jina la Ostaz Juma Namusoma. 

Kwa mujibu wa kinywa chake mwenyewe Ostaz Juma Namusoma,  juzikati nilipata nafasi ya kumbana na kunieleza kiunagaubaga namna alivyoweza kujipenyeza hadi kupata jina kupitia muziki wa Bongo. 
Ostaz Juma Namusoma akiwa kwenye ubora wake.

Kwa kinywa chake aliniambia kwamba, muziki kwake ni sehemu ya maisha ambayo ameishi kwa kipindi kirefu sana, kwani tangu alipokuwa mdogo alipenda muziki kushinda kitu chochote, msikie mwenyewe. 

OSTAZ JUMA: Mimi ni miongoni mwa vijana wa kipindi hicho ninayetokea Musoma mkoani Mara. 

Nilianza kupenda muziki tangu nasoma shule ya msingi tena mapema kabisa nikiwa darasa la tatu. Nikiwa shuleni nilikuwa napenda sana kuimba nyimbo mbalimbali za wasanii wa Kongo hadi  nikafi kia hatua ya kununua redio na kuwarekodi watoto wenzangu wakiimba kisha nazitunza nyimbo walizokuwa wakishindana kuimba hasa za Boringo za Wazaire.
Ostaz Juma Namusoma.

 Nimefanya hivyo hadi nikawa nagombezwa na wazazi wangu lakini sikukoma hadi nilipokuwa mtu mzima na kuanza kujifanyia mambo yangu ambapo wazazi hawakuweza kuniingilia. 

Kwa jinsi hii ndiyo utaweza kugundua kuwa nina kipaji cha kusimamia watu ndiyo maana nimeweza kuwasaidia wanamuziki wengi tu kwenye dansi ambapo kabla ya kujiingiza katika Bongo Fleva niliwahi kuwasaidia wanamuziki wa dansi kama Ally Chocky, Super Nyamwela, Jose Mara, Kalala Junior, Nyoshi ElSaadat, Mwinjuma Muumini na Mulemule. 

Tabia za wanamuziki kiukweli hazipishani sana hivyo ukiona meneja yeyote analalamika juu ya wanamuziki basi ujue matatizo yao mara kadhaa yamekuwa hayapishani sana, ila wanaopishana tabia na namna ya kuongoza ni mameneja tu.

 Namna ya kuongoza na kummeneji mtu kunategemeana na uwezo wa kifedha na akili pia, nasema hivyo kwa sababu muziki wetu umekuwa ukiyumba mara kadhaa kutokana na baadhi ya mameneja kuwa wasimamizi wabovu na wengine wanasimamia wakiwa hawana fedha ya kuweza kuwaongoza wasanii. 

Meneja ninayeweza kumpa saluti hapa Bongo ni Saidi Fella kwani ameonesha njia kubwa ya

kuimarisha Muziki wa Dansi na sasa umeanza kuwa juu  kiasi cha watu kuanza kuupenda tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ulianza kupoteza dira. ALIANZAJE KUSIMAMIA BONGO FLEVA? OSTAZ JUMA: 

Kwenye Bongo Fleva niliingia baada ya kuanza kumsimamia shemeji yangu aitwaye Abdallah David aliyekuwa akijiita Fil David, huyu nilijikuta namsimamia baada ya kumuona ana kipaji kizuri na baadaye nikaanzisha rasmi kampuni yangu ya Mtanashati. 
Ostaz Juma katika ubora.

Mtanashati ilipoanza tu nikapunguza kuwasaidia wanamuziki wa dansi hivyo nikajikita kwenye Bongo Fleva ambapo nilianza kumsimamia marehemu Sharo Milionea aliyemleta Kitale, lakini kabla sijaingia mkataba na Sharo akafariki dunia. 

Baada ya kufariki kwa Sharo Milionea ambaye ndiye msanii naweza kujisifi a katika upande wa Bongo Fleva kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana, nilimchukua PNC, Dogo Janja na Happy Balis ambao nilifanyanao project kibao kiasi ilifi kia hatua nikawa nakosana hadi na mke wangu kisa muziki huu. 

Ostaz Juma Namusoma

Nimekuwa nikiwasaidia wasanii hawa kwa muda lakini nilichoweza kujifunza ni kwamba wasanii wengi hawana adabu kabisa, kwani kuna siku niliwahi kukosana na mke wangu kwa kushindwa kumpeleka hospitali kisa kumpeleka Dogo Janja kwenye interview jambo ambalo mke wangu amekuwa akinikumbusha kila mara nami huwa halitoki kichwani hadi leo. 

Fedha niliyowahi kutumia hadi leo kwa ajili ya Dogo Janja na PNC naweza kujenga hata ghorofa tatu hapa mjini, lakini kwa kuwa nilikuwa naupenda muziki ndiyo maana leo utaona inafi kia muda sasa nimeamua kuachana na hawa Bongo Fleva maana hawana nidhamu hata tone ila ukilinganisha na wanamuziki wa dansi utagundua ni bora dansi kuliko Bongo Fleva. 

Nasema wanamuziki wa dansi ni bora kuliko wa Bongo Fleva kwa sababu wakati nadili na wanamuziki wa dansi walikuwa wanaonesha nidhamu ya hali ya juu jambo ambalo wanalifanya hadi sasa. 

Ujue nilikuwa nikiwapatia fedha za kodi za nyumba, mara nyingine kama Christian Bella na Chocky hawa niliwahi hata kuwalipia studio mara kadhaa kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao binafsi. 

Christian Bella yeye aliwahi hadi kunitungia wimbo ambao unaitwa Ubinadamu ambao hata yeye ukimuuliza leo anaujua na ninao mimi mwenyewe.

 Wasanii wakijua kuwa muziki ni kazi na sehemu ya maisha yao basi hakuna Bongo Fleva atakuja kushindwa kufanya mambo makubwa kama anavyofanya Diamond kwani kinachomfanya kuheshimika na kufanikiwa ni nidhamu yake tu.
Ostaz Juma Namusoma

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...