Wednesday, May 30, 2012

CHARLES TAYLOR ASUKUMWA JELA MIAKA 50

Charles Taylor mahakamani.

Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50 jela na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita. Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.

Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80.

Mwandishi wa BBC aliyeko The Hague Anna Holligan anasema rufaa dhidi ya hukumu hii huenda ikachukua miezi sita.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu.

Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.

Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani. Charles Taylor amelalamikia upande wa mashtaka kwa kuwatisha mashahidi katika kesi dhidi yake.

Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kuwapa silaha waasi na kubadilishana na almasi. Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kuhudimia kifungo chake nchini Uingereza.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMKARIBISHA MAKAMU WA RAIS WA IRAN KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Mei 30, 2012. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Iran Mhe. Mohammad Reza Rahimi,wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam, leo Mei 30, kwa ajili ya mazungumzo, Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.Kulia ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales LAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Mei 30 2012, (kulia) ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam (kushoto) ni Mkarimaniwa Makamu wa Rais wa Iran.Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo, Mei 30, 2012 Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.


Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, akiweka saini katika kitabu cha Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) wakati alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo leo Me 30, 2012. Kulia ni Waziri wa Kazi wa Iran, Sheykhales Lam. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo, Mei 30, 2012 kwa ajili ya mazungumzo. Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajil ya ziara ya kikazi ya siku tatu..


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo, Mei 30, 2012 Makamu wa Rais wa Iran amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
WAZIRI ABOUD NA MAASKOFU WA TANZANIA WAJADILI VURUGU  ZANZIBAR OFISINI KWAKE

Askofu Mkuu wa Tanzania Dk.Costantino Mokiwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud, walipofika Ofisi hapo kwa ajili ya mazungumzo na Waziri kuhusiana na vurugu zilizoyokea wiki iliopita na kusababisha uharibifu na uvyunjaji wa makanisa katika sehemu mbalimbali na mali za baadhi ya wananchi kuharibiwa.kutokana na vurugu hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud, akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Makanisa Tanzania ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Tanzania Dk. Mokiwa, uliofika Ofisini kwake kwa mazungumzo.mjini Zanzibar.

Maaskofu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,akitowa maelezo kwa ujumbe huu ulipofika Ofisini kwake Vuga.



Waandishi wakiwa katika harakati za kazi zao ili kuwahabarisha Wananchi mambo yaliokuwa yakizungumzwa katika mkutano huo

Tuesday, May 29, 2012

CHADEMA-WABUNGE NA VIONGOZI WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI


Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamtembelea rasmi Balozi wa Tanzania nchini Marekani.


Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

Wabunge wa Chadema Mhe. Peter Msigwa wapili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo Janja, (Watatu kulia), ofisa wa ubalozi Mhe. Peter Msigwa, Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc wakipata picha ya pamoja na balozi Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Nchini Marekani.

Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc. (Picha na swahilivilla.blogspot.com)


WEMA SEPETU AVISHWA PETE NA MWINYI KUTOKA MACHOZI BAND @NEW MAISHA CLUB USIKU HUU





Peter Moe & Gadna G Habash


Mateja & Snura


Sam Machozi, Snura & Sharo Millionaire


Jamillar, Chaz Baba & Snura


Abra & Choka wakipata shisha




Wema Sepeta na Bodyguard wake


Wema & Abou


mmmmh....












Jini Kabula





Mtu mzima Mwinyi akaenda chini pwaaaa...


Akakumbatiwa watu weweeeeeee


Heeeh si akaweka pete kidoleni pale kabaaaaaaa

Mabusu hihaaaaa, watu pipooooo

The End...

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...