Tuesday, January 19, 2016

MUUZA UNGA MAARUFU AKAMATWA DAR!


Mfanyabiashara maarufu jijini Dar ‘kigogo’, Daudi Yakubu Kanyau anayehusishwa na biashara ya unga.

Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara maarufu jijini Dar ‘kigogo’, Daudi Yakubu Kanyau (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Makao Makuu Ufundi, Kilwa Road, Dar akihusishwa kwa namna moja au nyingine na biashara ya madawa hayo maarufu kwa jina la ‘unga’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mfanyabiashara huyo alikuwa akitafutwa na dola kwa kufuatilia nyendo zake siku nyingi baada ya kuwemo kwenye orodha ya watu wanaosadikiwa kuijua kiundani biashara hiyo.

Nyumba aliyomjengea mtumishi wake.

TAARIFA NDANI YA JESHI LA POLISI
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa Kanyau alikamatwa nyumbani kwake, Salasala jijini Dar wiki moja iliyopita kwa ushirikiano wa kikosi cha madawa ya kulevya na kikosi cha kupambana na utakatishaji fedha haramu (money laundering) ambao wao huchunguza utajiri wa mtu na uhalali wa kipato.

MALI ZAKE ZASHIKILIWA
Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi hilo zinadai kuwa polisi wanashikilia mali za Daudi kwa ajili ya uchunguzi wa namna alivyozipata pia kuchunguza misaada mbalimbali aliyokuwa akiitoa kwa jamii, kama vile kujenga nyumba za familia, ibada na mingine.

KWA NINI?
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutangaza vita dhidi ya wauzaji na watumiaji wa unga na kuagizwa kukamatwa mara moja, wakiwemo wale wanaoshukiwa.


Moja ya gari lake linaloshikiliwa.

DCI ANENA
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania, Diwani Athumani hivi karibuni aliliambia gazeti hili kuwa msako mkali umeanzishwa na watu wengi wamekamatwa, wakiwemo vigogo lakini hakuwa tayari kutaja majina yao hadharani kwa madai kwamba upelelezi bado unaendelea.

ALIWAHI KUKAMATWA UWANJA WA NDEGE
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilizungumza na kamishna mstaafu, SACP Godfrey Nzowa ambaye alikuwa bosi wa kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya ambapo alisema miaka mitatu iliyopita, yeye aliwahi kumkamata Kanyau kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar.

HUYU HAPA NZOWA MWENYEWE
“Mimi niliwahi kumkamata Kanyau miaka kama mitatu iliyopita pale uwanja wa ndege akitokea nje ya nchi na tulifuatana naye hadi kwake, Magomeni Mapipa (wakati huo). Tulifanya upekuzi nyumbani kwake lakini hatukupata kitu. Wananchi wamekuwa wakitupa taarifa kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo ndiyo maana tulimkamata na kumpekua,” alisema Nzowa.

DCP Boaz.

Kamanda Nzowa alisema anaamini kuwa katika serikali hii ya Rais Magufuli ‘JPM’ vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo watakimbilia nje ya nchi maana kumekuwa na ushirikiano mkubwa wa vyombo vya dola.

UWAZI LATINGA KILWA ROAD
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilifika makao makuu ya kitengo hicho na kumkuta Kanyau akishikiliwa huku akiendelea kuhojiwa. Mama yake mzazi, dada zake na ndugu wengine walikuwepo.

Mama mzazi wa Kanyau alisikika akisema anashindwa kulala kwa sababu ya kukamatwa kwa mtoto wake huyo. Alidai kwamba hawezi kula bila kumuona mwanaye ndiyo maana amekuwa akifika hapo kwa lengo la kula naye, pia kuona kama kuna uwezekano wa kumuwekea dhamana.

MKUU WA KITENGO NA UWAZI
Uwazi lilizungumza na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Robert Boaz ambaye amechukua nafasi ya Nzowa. Boaz alikiri kukamatwa kwa Kanyau na kusema bado anaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

“Nisingependa kuzungumzia suala la Kanyau kwa kipindi hiki maana upelelezi bado unaendelea na kuna uwezekano wa kutoa taarifa zaidi kwa vyombo vya habari, lakini sisi kama jeshi la polisi tunaomba ushirikiano wa karibu na wananchi kuwafichua watu wote wanaojihusisha na biashara hii haramu.

“Mlango wangu upo wazi saa zote hivyo nawaomba raia wema wajitokeze kutupa taarifa zitakazosaidia katika mapambano dhidi ya wanaojihusisha na madawa ya kulevya. Tunaahidi hakuna siri itakayotoka kwa watakaotupa ushirikiano,” alisema Kamanda Boaz.

BAADHI YA VIGOGO POLISI WATAJWA
Habari zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni zinadai kuwa baadhi ya vigogo wa jeshi la polisi wamekuwa wakitajwa kujihusisha na biashara ya kuuza unga huku wengi wao wakikamatwa, wengine wakiamua kuacha kazi wenyewe.

“Hao wanaokamatwa kwa kuhusishwa na biashara ya unga, ujue wapo na baadhi ya viongozi wa polisi. Kuna waliokamatwa, lakini wengine sasa kwa kuona hali mbaya wameamua kuacha kazi wenyewe,” kilisema chanzo chetu kimoja kutoka jeshi hilo.
Habari hii inaendelea kufuatiliwa.
25

HAPPY BIRTHDAY OSTAZ JUMA NAMUSOMA

Leo ni siku pekee ya furaha kwa rafiki na bosi wangu wa karibu Ostaz Juma Namusoma, ambapo leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Ostaz Juma amesema kwamba hana mpango wa kufanya sherehe kubwa leo zaidi  jioni ya leo anatarajia kuketi na familia yake na kukata keki  kwa pamoja nyumbani kwake Mbezi.
HONGERA SANA OSTAZ JUMA NA MUNGU AKUZIDISHIE MAISHA MAREFU NA YENYE BARAKA SIKU ZOTE. 
Ostaz Juma Namusoma akiwa katika pozi.


Friday, January 1, 2016

Ray C, kama ni kweli unamuaibisha JK kwa makusudi


Rehema Chalamila Ray C.

MIONGONI mwa wasanii ambao wanabeba nembo ya Muziki wa Kizazi Kipya upande wa wanawake, huwezi kuacha kulitaja kwa kujiamini kabisa jina la Rehema Chalamila, ambaye mashabiki wanamtambua zaidi kama Ray C.

Alifanya kazi kubwa, siyo tu kuonesha kuwa wanawake wanaweza, bali pia kuthibitisha kiasi kikubwa cha ubora wake katika tungo, uimbaji na zaidi, uwezo wa kutumia mwili wake kuvutia mashabiki kwa kuonesha manjonjo jukwaani.

Jambo hili lilisababisha kupata wafuasi wengi ndani na nje ya nchi kiasi cha wakati f’lani kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa kike waliokuwa wakialikwa katika matamasha kwa bei mbaya, enzi ambazo yeye, Lady Jaydee, Stara Thomas na Unique Sisters walikamata Bongo Fleva.

Huenda, uwezo wake huo, uliomfanya kukutana na watu wengi katika maeneo mbalimbali, ndiyo uliomfanya akaanza kubadili aina ya maisha yake, kutoka yale aliyozoea hadi mapya, ambayo kwa bahati mbaya, yanaelekea kumaliza enzi zake zitakazobaki historia.

Upo ushahidi wa wazi kuwa binti huyu, akiwa kileleni kabisa mwa mafanikio yake, alijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya, ujinga ambao unafanywa na wasanii wengi wa Muziki wa Kizazi Kipya, wenyewe wakidhani kwa kufanya hivyo, wanaonekana kuwa wajanja na watoto wa mjini, wakati ukweli ni kinyume chake.

Baada ya picha zilizonaswa akiwa yuko bwii kutolewa gazetini, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alijitolea kumsaidia, kwani alikumbuka mchango wake mkubwa katika Bongo Fleva.

Baada ya kupata matibabu na kufikia unafuu wa kuridhisha, akiwa na mama yake mzazi, Ray C alikwenda Ikulu mjini Dar es Salaam kumshukuru Kikwete kwa msaada wake mkubwa na kuahidi kwa umma kuwa asingerejea tena kwenye kubwia unga.

Hata baada ya kuwa bado anaendelea kupata matibabu ya kumsaidia kuachana na matumizi hayo ya unga, yapo madai ya chinichini kuwa msanii huyo aliyewahi kubatizwa jina la Kiuno Bila Mfupa, anaendelea kula ‘ngada’.

Wanaodai hivyo ni watu wake wa karibu, ndugu zake na hata watu ambao wamemsaidia sana kumrejesha katika ‘dunia’ inayotakiwa.

Tunawajua watu wengi waliotumia unga na kuathirika vibaya, lakini baada ya kusaidiwa kujitambua, waliamua kwa dhati kufuata masharti ya dozi na hatimaye wamepona kabisa na wanaendelea na kazi za ujenzi wa taifa kama kawaida.

Anaweza kukataa kwa nguvu kubwa kuwa ameacha kula ‘sembe’, lakini utumiaji wa madawa uliokithiri haujifichi, hata kwa mwonekano tu wa kawaida humtambulisha, ndiyo maana mateja wote wa unga muonekano wa sura zao unafanana!

Nimshauri tu kwa nia njema kuwa ulaji unga haujawahi kusaidia maisha ya mtumiaji yeyote, awe staa au raia wa kawaida. Kwa taarifa yake, wajanja wote wanaukimbia unga na kuwaachia mafala, ndiyo maana kila siku wanabakia kuwa ombaomba, wadokozi na baadhi yao kufanya uhalifu unaokatiza maisha yao.

Ingawa kila mtu ana haki ya kuachwa kuishi maisha yake binafsi, lakini baadhi ya staili, licha ya kuwa ni uvunjaji wa sheria, pia hazikubaliki. Ni mjinga pekee ndiye anaweza kujivunia staili ya maisha inayomaliza uwezo wake wa kufikiri, kutenda na hata kuendelea.

Na sisi wengine, hatupaswi kukaa kimya tunapoona mtu mwenye uwezo wa kujiendeleza yeye binafsi na jamii inayomzunguka, akijimaliza makusudi. Huenda alianza kuvuta akiwa hajui athari zake kwa vile alikuwa bado ‘mshamba’, lakini vipi leo aendelee hata baada ya kushtuliwa kuwa unga ni soo?

Ray C, kama yanayosemwa ni kweli, jitazame upya kwani kujiingiza kwenye unga tena ni kumuabisha Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.

ETI KIDOA AMTANGAZIA VITA ZARI KWA DIAMOND!?


Video Queen maarufu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’.

Musa mateja
Video Queen maarufu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ amemtangazia vita mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ akidai atafanya kila njia amnase msanii huyo.

Rafiki wa karibu wa Kidoa aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alidai kuwa, Kidoa alikuwa akimpenda sana Diamond hata kabla ya kuwa na Zari ndiyo maana ana ndoto za kuwa naye.

“Kidoa anamzimia sana Diamond, achilia mbali kumpenda kutokana na kazi yake ya muziki lakini pia kimapenzi, maana kuna wakati anakosa raha kabisa anapowaona Zari na Diamond wakiwa kimahaba,” anadai mtoa habari huyo.

Katika kujua ukweli wa habari hii, mwandishi wetu alimtafuta Kidoa ambapo bila kuficha alianika hisia zake kwa kusema: “Kiukweli nampenda sana, najua Zari hawezi kujisikia vizuri kusikia maneno haya lakini ndiyo hivyo na niko tayari kwa lolote…

“Nilipotangazwa kuwa msanii mwenye mvuto kwa mwaka 2015, kama ilivyokuwa kwa Wema mwaka 2013, nilijiona mwenye vigezo vya kuwa naye, si yeye ni sukari ya warembo? Na mimi napenda sukari.”

Hivi karibuni Kidoa na Diamond walikutana ndani ya Ukumbi wa Dar Live na kufanikiwa kuongea, kupiga picha na kubadilisha namba za simu, jambo lililotafsiriwa na wadaku kuwa, Zari akilemaa, ameliwa.
Mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’.

CHRISTIAN BELLA AUANZA MWAKA KWA KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA MBAGALA

Christian Bella akipanda jukwaani kuwasalimia mashabiki.Mashabiki wakijiachia kwa kucheza muziki dakika chache kabla ya kuanza mwaka mpya 2016Ni full kufurahia.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za mkononi, Airtel Tanzania na wafanyakazi wa Dar Live wakiandaa maputo kwa ajili ya shamra shamra za kuukaribisha mwaka mpya 2016.
Maputo yakipeperushwa hewani kuashiria kuanza mwaka mpya 2016.
Bella akitoa kionjo wakati wa kuukaribisha mwaka mpya.
Christian Bella (mwenye kofia nyekundu) na Mama Tunu wakitikisa chupa za shampeni. Wanaoshuhudia tukio hilo ni mashabiki pamoja na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo (katikati mwenye shati la dratfi).
Zoezi la kufungua shampeni likishika kasi.
Shampeni ya mama Tunu hiyooooo ikafunguka.
Bella naye akakazana.
Dakika zikatimia…. mwaka 2016 huoooo ukafika.
Bella akaanza kuwaonjesha shampeni mashabiki zake.
Mashabiki wakichukua picha za ukumbusho wa tukio hilo kwenye simu zao.
Bella akaanza kutoa vionjo vya nyimbo zake kali.Bella acha kabisaaaaa
Mashabiki wakifuatilia shoo hiyo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...