Akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwake.
Amesema kuwa zoezi hilo linaonyesha ni jinsi gani wafanyakazi wa TAZARA wamekuwa wakiguswa na maswala mbalimbali ya kijamii hususani swala la ukosefu wa Damu mahospitalini huku akiyataka mashirika mengine na watu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachangia damu mara kwa mara wawezavyo kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wamaopoteza maisha yao kwa kukosa Damu.
Aidha mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa damu kutokana na kuongezeka kwa maswala mbalimbali yakiwemo ya ajali,vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua wanaofariki kwa kukosa damu,na magonjwa mengine mengi hivyo akawataka watanzania kujitahidi na kuhakikisha kuwa angalau wanachangia damu kwa mwaka japo mara mbili ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.
Zoezi la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA ambapo wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine wamejitokeza kucnagia damu (PICHA NA EXAUD MTEI MSAKA H |
Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizungumza na wanahabari wakati wakiendelea na zoezi la uchagiaji wa Damu. |
No comments:
Post a Comment