AZAM TV kupitia
chaneli yake ya Sinema Zetu, mapema leo imezindua rasmi ‘projekti’ iliyopewa
jina la Kiwanda cha Filamu, na kipindi kipya kiitwacho Taxi, vyenye lengo la kuibua vipaji vya wasanii wa
maigizo na wapiga picha za video
chipukizi.
Projekti hiyo
ambayo ilianzishwa mwanzoni mwa Machi mwaka huu ilitoa furasa kwa watu
mbalimbali ambao wangependa kushiriki kutuma kazi zao na wamepatikana zaidi ya
washiriki 200.
Akizungumza na wanahabari
katika uzinduzi huo kwenye ofisi za Azam zilizoko eneo la Tazara jijini Dar,
Msimamizi wa Uzalishaji wa Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa, alisema washiriki hao
watawachuja chini ya majaji akiwemo muigizaji wa siku nyingi hapa nchini, Suzan
Lewis ‘Natasha’, ili kuwapata washiriki 22.
Baada ya kupatikana,
watapatiwa mafunzo mafupi kisha wao pamoja na mastaa wa filamu hapa nchini
watashiriki kwenye tamthilia itakayojulikana kwa jina la Taxi.
Nzowa alisema:
“Washiriki ni kuanzia umri wa miaka 18 na kesho Jumatano pale Coco Beach ndipo
tutaanza kufanya mchujo wa awali ambapo mpaka mwisho tunatarajia kupata
waigizaji 20 na wapiga picha wawili ambao watashiriki kwenye tamthilia ya Taxi
ambayo itazinduliwa Julai mwaka huu na itakuwa ikionyeshwa katika chaneli yetu
ya Sinema Zetu.”
Mrope Kiwanga, akifafanua zaidi namna projekti hiyo itakavyonufaisha watu wengi.
Zamaradi Nzowa akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa projekti hiyo.
Muigizaji Suzan Lewis ‘Natasha’, (kushoto) akimlisha keki msanii na mtangazaji mahari Bongo, Daniel Kijo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wahusika wa tukio hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
Muigizaji Issa Mbura (kushoto) akimlisha keki Natasha.
Mwandishi wa gazeti la Championi, Mohamed Mdose (kushoto) akilishwa keki na Natasha.
No comments:
Post a Comment