MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Mama Kijacho Khalid
Ramadhani ‘Tundaman’’ hatimaye amepata dili la ubalozi wa kampeni ya
kuhamasisha wanawake wa Africa kuhusiana na tamasha la wanawake liitwalo (AFWAB
AMSHA MAMA2016).
Tamasha hilo ambalo lilianza tangu mwishoni
mwa Desemba mwaka jana, kunako Hoteli ya nyota tano ya The Tribe na vitongoji
vya Nairobi, Kenya, mfanyabiashara mashuhuri na mwenye jina kubwa music , alifanya
bonge la tamasha liliacha gumzo kwa kuvuta maelfu wa watu kutoka kila kona ya
dunia.
Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy
na Candy Records,
Joe Kariuki, aliratibu tamasha maridadi lililojulikana kama Amsha Mama,
maalum kwa Wanawake wa Kiafrika, tamasha lililofanyika katika Hoteli ya
kifahari ya Tribe, sehemu ambayo ni maarufu sana pia kwa wasanii kutoka Marekani,
akiwemo Akon.
Mkurugenzi Mtendaji wa ‘lebal’ ya Candy
na Candy Records,
Joe Kariuki akiwa katika pozi. |
Tamasha hilo ambalo lengo kubwa lililenga kuzungumzia bayana hali halisi ya
maisha ya mwanamke wa Afrika kuhusu safari yake, mapigano yake kimaisha,
mafanikio, biashara, ubunifu na ushindi wake katika maisha.
Kama mwanaume ambaye siku zote aliye karibu na moyo wa mwanamke ambaye alitaka kumtuza ama kumzawadia kwa
hatua aliyofikia, kumtia moyo, kumhamasisha katika safari yake ya mafaniko
katika jamii hii yenye mfumo dume barani
Afrika.
Akizungumza katika event hiyo, Joe
alisema: "Kuwawezesha wanawake ni muongozo
katika jamii, nami nataka kutumia ujuzi wangu na uzoefu nilionao kujenga
jukwaa kwa ajili ya wanawake kukua biashara zao."
Washiriki wengi ambao ambao wengi
wao walisafirishwa kutoka nchi za mbali kwa ajili ya kuhudhuria ‘event’
hiyo, waliunga mkono mawazo ya Joe, mfano Uganda na Italia.
Lisa raia wa Italia alisema: "Dhana ya Amsha Mama ni ya kipekee. Naangalia
wanawake wenye uwezo wa kuzalisha hila zitakazotumika huko Milan. "
Sophie kutoka Uganda, alisema: "Ninawezaje ku-miss hii! Kama mwenyekiti
wa chama chetu cha wanawake 600 nataka kuhakikisha wanapata aina hii ya fursa
kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zao na kwa ajili ya kupata mtandao na wanawake
wengine."
Rundo la wanawake waliokuwa na hisia kama hizo, akiwemo mwingine kutoka Copenhagen, Denmark: "Tamasha
haya ndiyo tunahitaji kwa ajili ya kukuza wanawake. Inaonyesha nguvu za
wanawake na mipango yao."
Na katika hilo, Joe anaendeleza jitihada zake za si tu kumwezesha Mwanamke wa
Afrika, bali pia kumuinua, kumtia moyo wake, kumpa mwangaza na kujihusisha
kwake.
Hivyokwa sasa na ndiyo maana ameandaa maonyeshwa makubwa ya wanawake (AFWAB
AMSHA MAMA 2016), yatakayofanyikia katika Uwanja wa Kedong ranch uliopo katika
jiji la Naivasha nchini Kenya Machi 25-27 2016.
No comments:
Post a Comment