Miongoni mwa mameneja Tanzania waliosaidia kuusimamisha muziki wa Bongo Fleva na Dansi, Ostaz Juma Namusoma. |
UKIZUNGUMZIA miongoni mwa wadau wakubwa wa muziki waliosaidia
kuusimamisha muziki wa Bongo Fleva na Dansi nchini ni wazi jina la Ostaz Juma
Namusoma litakuwa miongoni mwa majina utakayoyataja.
Kabla ya kuwasimamia wanamuziki wa Bongo Fleva, Ostaz Juma Namusoma alikuwa
akiwasaidia sana wanamuziki wa Dansi kama vile Ali Chocky, Super Nyamwela, Jose
Mara, Kalala Junior, Nyoshi El-Saadat, Christian Bella, Mwinjuma Muumini na
wengine wengi.
Ikumbukwe kuwa hata Wimbo wa Ubinadamu ulioimbwa na Christian Bella
ulikuwa maalum kwa mdau huyo wa muziki. Ostaz Juma aliamua kuupa kisogo muziki
wa Dansi na kujikita kwenye Bongo Fleva ambapo alianzisha Kampuni ya Watanashati
iliyokuwa na vichwa kama vile, PNC, Marehemu Sharomilionea,Kitale, Suma
Mnazareti pamoja na Dogo Janja.
Wasanii hao wote kwa sasa hawapo chini yake kutokana na kila mmoja kuondoka
kwenye kampuni hiyo na huku nyuma yake akimwagia maneno mbofumbofu na kejeli nyingi kwa mdau huyo na baada ya
muda tangu watoke walijikuta wakishindwa kuendana na soko la muziki.
Katika makala haya yanawachambua wasanii hao ambao mzimu wa Ostaz Juma
bado unazidi kuwatesa.
Msanii wa Bongo Fleva aliyewahi kuwa chini ya usimamizi wa Ostaz Juma Namusoma kupitia kampuni ya Mtanashati PNC akiwa katika pozi. |
PNC
Pancras Ndaki kama anavyojulikana kwenye cheti chake cha kuzaliwa,
anaingia kwenye listi ya wasanii waliopitia kwenye mikono ya Ostaz Juma na
kupata kusikika vilivyo.
PNC alikaa na Ostaz Juma kwa muda mrefu na kuamua kujitoa huku sababu
akiitaja ni mambo kumwendea mrama kwa kuwa alikuwa akijaribu kutoa nyimbo za
kila aina kulishawishi soko gumu la muziki wa Bongo Fleva lakini mambo hayakuwa
sawa.
Aliamua achukue uamuzi mgumu wa kujiondoa na kuanzisha kundi la Top
Fleva huku akidai alikuwa hapati msaada wowote kwa bosi wao (Ostaz Juma) na
kwamba anawasema vibaya kwenye media. Baada ya kusema hayo tu miezi michache,
PNC alirudi na kumpigia magoti Ostaz Juma kumuomba msamaha na kwamba amrudishe
kundini.
Msanii aliyekuwa chini ya usimamaizi wa Ostaz Juma Namusoma kupitia kampuni ya Mtanashati Suma Mnazareti katika pozi. |
Suma Mnazareti
Suma Mnazareti naye ni miongoni mwa wasanii wanaoendelea kuandamwa na
mzimu wa Ostaz Juma baada ya kujitoa.
Kwa mujibu wa Suma, aliamua kujitoa kwa sababu alikuwa akikosa kile
alichokuwa akitarajia na pia aliona kama Ostaz anawajali sana wasanii wa muziki
wa Dansi japokuwa alikuwa amejikita kwenye Bongo Fleva.
Baada ya kujitoa kwake alifanikiwa kutoa wimbo na Ommy Dimpoz uitwao
Chukua Time ukafanya poa sana kisha Tuko Wangapi akiwa na Tunda Man nao ukafanya
poa huku akitoa vijembe kwa Ostaz Juma.
Baada ya hapo, mzimu wa Ostaz Juma ukaanza kumtesa na kujikuta akishindwa
kurejea kwenye soko la muziki na kila kazi aliyokuwa akiitoa ilikuwa ikibuma
hadi sasa.
Dogo Janja. |
Dogo Janja
Abdulaziz Abubakari ama Dogo
Janja kwa jina la kisanii, alichukuliwa na Ostaz Juma baada ya kuachana na
kundi la Tip Top ambapo alijiunga na wenzake ambao ni PNC pamoja na Suma Mnazareti
na kufanikiwa kutoka na wimbo wa pamoja ulioitwa Watanashati.
Baada ya kukaa kwa kipindi kirefu, Dogo Janja alitimuliwa na Ostaz Juma
kwa sababu iliyoelezwa ni kukosa heshima na pia kukimbiwa japokuwa alimtafutia
shule ambayo alishindwa kusoma.
Dogo Janja aliamua kurudi Tip Top chini ya Madee lakini napo mzimu wa
Ostaz Juma uliendelea kumtesa ambapo inaelezwa kuwa hadi sasa ameingia katika
mtafaruko mkubwa baada ya kudai kuwa ana kazi zaidi ya 10 ambazo anabaniwa
kuzitoa huku akirandaranda mitaani pasipo ishu yoyote.
Ostaz Juma Namusoma katika pozi. |
Msikie Ostaz Juma
Over The Weekend ilifanikiwa kuzungumza na Ostaz Juma juu ya wasanii
hao ambapo alifunguka;
“Ujue sisi wadau wa muziki huwa tunaandamwa sana na maneno hasa pale
unapoachana na msanii uliyekuwa ukimsaidia. Nimewahi kuwasaidia wasanii wengi
kwa mfano ukiangalia mimi na Fella (Said Fella) tunawasimamia wasanii kwa pesa
zetu za mfukoni tofauti na mameneja wengine ambao wamekuwa wanasimamia wasanii kwa manufaa yao kama hawapati basi wanaachana
na wewe.
“Wasanii hao (Suma, PNC na Dogo Janja) nawatambua kama wasanii
waliopitia kwenye mikono yangu, japokuwa kila mmoja aliamua kuondoka lakini
naendelea kuwasaida pale wanapokwama hadi leo.
Kweli juzikati nilibahatika kuwa miongoni mwa watanzania wengi
niliyesikiliza sauti ya Dogo Janja akiongea na msaichana mmoja huku akitoa
lawama kubwa kwa wasimamizi wake wa sasa ambao wamekuwa naye kwa muda mrefu
sasa tangu atoke kwangu.
Record hiyo kweli imenisikitisha sana baada ya kumuona kijana wangu
akilalama kiasi hicho lakini kikubwa nilichokigundua hapo ni kwamba, mameneja
wengi wa wasanii wetu ni tatizo maana wamekuwa wakiwachukua wasanii ili wao
wanufaike badala ya kuwasaidia kama nilivyokuwa nikifanya mimi na Said fella.
Kusema kweli kwa haya maneno ya Dogo Janja naanza kuona wazi kabisa
kuwa Babu Tale na Madee hawana uwezo wa kummeneji msanii hasa asiyekuwa na
fedha maana wao wanataka pesa kutoka kwake huku msanii mwenyewe amekuwa
akihitaji msaada wa kikazi na fedha.
Boss wa Mtanashati Ostaz Juma Namusoma katika pozi. |
Mimi suala la mzimu wangu kuwasumbua kweli nimekuwa nikiambiwa na wengi
hata baadhi ya wasanii hawa kama PNC juzi kati aliwajhi kuniambia kitu kama
hicho, tena akisema kweli mkono wangu si wakuacha vibaya kwani karibia wote
niliowahi kuwasimamia wameshindwa kuendelea nje ya Mtanashati na zaidi
wanmebaki wakitabika kama unavyomuona Dogo Janja leo hii.
PNC alikuwa akiniambia kuwa kwenye maisha jhakuna mtu asiyekuwa na
mapungufu ila mimi kwake nitabaki kuwa kama lulu ya mafanikio kwani pamoja na
yeye kutoka kwangu kwa mwembwe nyingi bado amekuwa akinihitaji kwa asilimia
kubwa sambamba na wengine wote akiwemo Dogo Janja ambaye ninamsaidia
anapokwama,” alisema Ostaz Juma.
Ostaz Juma Namusoma. |
No comments:
Post a Comment