Monday, February 1, 2016

HILI NDILO DUKA LA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC.


Rais wa Simba Bw. Evans Aveva leo amezindua rasmi duka la Simba ambalo litakuwa likiuza vifaa vya michezo, jezi, kofia, T-shirts pamoja na vitu vingine vingi vyenye nembo ya Simba kwa ajili ya kujiingizia kipato kutokana na nembo ya timu yao.
Imekuwa muda mrefu sasa tangu vilabu hivyo viwili vya Simba na Yanga vilipoanza kupiga kelele za kuhakikisha bidhaa zenye nembo za klabu zao zinavinufaisha vilabu lakini bado wajanja waliendelea kufaidika kutokana na vilabu hivyo kushindwa kudhibiti watu ambao wamekuwa wakipiga pesa kwa kuuza bidhaa zenye nembo za vilabu hivyo.
Hiyo ni changamoto kwa vilabu vingine vya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambavyo bado vimelala huku wajanja wa mjini wakiendelea kuponda pesa kutokana na kuuza bidhaa zenye nembo zao huku wao wakiwa hawapati hata shilingi 100.
Rais wa klabu ya Simba (katikati) akikata utepe kuzindua duka la kuuza vifaa vya Simba lililopo Dar Free Market Mall Ground Floor

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...