Kikosi cha timu ya Simba kikicheza mchezo wake wa 15 kwenye ligi kuu Tanzania bara, jana kilifanikiwa kuifunga timu ya JKT Ruvu mabao 2-0
Magoli
yote yalifungwa katika kipindi cha pili ambapo goli la kwanza lilifungwa na
mshambuliaji wa kimataifa Hamisi Kizza katika dakika ya 51 baada ya mshambuliaji
Danny Lyanga kufanyiwa madhambi ndani ya boksi la timu ya JKT, kwa ustadi
mkubwa Hamis Kizza alifunga penati hiyo na kufikisha jumla ya magoli 10 tangu
kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2015/2016. Goli la pili lilifungwa na
mshambuliaji Lyanga dakika ya 61 baada ya pasi nzuri iliyotoka kwa beki wa
kulia Nimubona ikamfikia Mkude na kumpasia Danny Lyanga ambapo aliwatoka mabeki
pamoja na kipa na kufunga goli. Mpaka kipenga cha mwisho kinapigwa JKT Ruvu 0 –
2 Simba.
Simbasports.co.tz
ilipata nafasi ya kuongea na kocha wa Simba Jackson Mayanja na kusema
“tumefurahia sana ushindi wa leo haikuwa mechi rahisi ilikuwa ni mechi yenye
ushindani mkubwa sana lakini kikosi changu kimeweza kupambana na hatimaye
kuondoka na pointi 3 muhimu, tunatoa shukrani kwa mashabiki wanaoendelea
kujitokeza kushangilia timu yetu kwa ajili ya kuhakikisha tunaendelea kupata
matokeo mazuri.
Simbaports.co.tz
inawapongeza wachezaji na benchi lote la ufundi kwa kazi nzuri ya leo
iliyoiwezesha timu kushinda.
Unataka
kuwa wa kwanza kupata habari za klabu yako ya Simba tuma neno Simba kwenda
namba 15460 utatumiwa ujumbe jibu “OK” nawe utakuwa umejiunga na huduma ya
Simba News. Huduma itakayokuwezesha kupata habari za Simba popote ulipo kwa
wateja wa Tigo na Vodacom.
Kikosi cha timu ya JKT Ruvu |
No comments:
Post a Comment