Thursday, January 28, 2016

MBWANA SAMATTA AWASILI UBELIGIJI TAYARI KWA KUITUMIKIA TIMU YAKE MPYA YA GENK

 Mbwana Samatta
STAA wa soka la Bongo Mbwana Samatta ‘Popa’ ameondoka usiku wa January 27 kuelekea Ubeligiji kujiunga rasmi na klabu ya Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubeligiji maarufu kama Belgian Pro League.
Akiwa tayari amesaini mkataba na klabu hiyo, Samatta alikuwa anasubiri ‘taa ya kijani’ kutoka kwa bosi wa TP Mazembe Moise Katumbi ambaye mwanzoni alikuwa anaweka ‘kauzibe’ kutoa ruhusa kwa mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika kwenda kujiunga na klabu ya Genk.
Samatta anatarajia kuanza maisha mapya kwenye klabu ya Genk baada ya kuipa mafanikio makubwa klabu ya Mazembe tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2011 akitokea Simba SC.
Atakumbukwa na wana-Lubumbashi kwa kuisaidia timu yao kutwaa taji la ubingwa wa Afrika mwaka 2015 pamoja na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kuifungia timu yao mabao saba kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.
Samatta 

Samatta ameshawasili nchini Ubeligiji tayari kwa ajili ya kuanza majukumu mapya kwenye klabu hiyo ya barani Ulaya.
Klabu ya Genk imeshawahi kuwatoa mastar wakubwa barani Ulaya wanaotamba kwenye vilabu vikubwa vya ligi maarufu duniani. Christian Benteke (Liverpool), Kelvin De Bruyne (Manchester City), Thibaut Courtois (Chelsea) ni baadhi ya majina ya mastar ambao wamewahi kupita kwenye klabu ya Genk.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...