Wednesday, January 20, 2016

KWA STYLE HII WEMA,ZARI WATAUWANA!


Wema Sepetu
 Hii sasa ni vita! Mpambano mkali umeibuka kwa mara nyingine kati ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Uganda,
The Boss Lady’ ambaye pia ni mzazi mwenzake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Mapambano hayo yameanzia kwenye mitandao ya kijamii kisha kuhamia mitaani kwa timu zao ambapo baadhi ya watu wanasema kuna kitu zaidi katika chuki ya Zari kwa Wema.
KUTOKA MTANDAONI
Ni Zari ambapo inadaiwa, mapema wiki hii alitupia kwenye akaunti yake ya Instagram maneno yaliyotafsiriwa ni kejeli kwa Wema. Aliandika: Fake car (gari magumashi), fake house (nyumba magumashi), fake men (wanaume magumashi).
Zari Hasan The Boss Lady
Kisha akatupia ujumbe akijifanya anawasiliana na wifi yake, yaani dada wa Diamond aitwaye Esma Platnumz akimuuliza: Umelipa Tanesco?
Wema aliwahi kudaiwa kuchezea mita ya Luku ya Shirika la Umeme (Tanesco) hivyo kusababisha deni la shilingi milioni tisa (9,000,000).
TAFSIRI ILIYOPO
Watu wanaomuunga mkono Zari (Team Zari) wameliambia Amani kuwa, ujumbe huo wa Zari ulimlenga Wema kwa sababu lile gari lake (Range Rover Evouge) alilotamba kwenye siku yake ya kuzaliwa kwamba amelinunua kwa shilingi milioni mia mbili (200,000,000), sasa hivi hana.
“Pia, Zari amesema fake house, kwa sababu Wema alisema ile nyumba aliyokuwa akiishi ya Kijitonyama, Dar aliyohama hivi karibuni kwenda Ununio, awali alisema ni yake. Pia, fake men kwa sababu hatulii na mwanaume mmoja kwa muda mrefu.
WEMA AJIBU MAPIGO
Wema hakuona sababu ya kukaa kimya, naye akatupia ujumbe akisema hawezi kujibizana na kibibi, yaani Zari, kwamba umri umemtupa mkono. Kwa sasa Zari ana miaka 35, Wema 28 na Diamond 26.
SHOGA MKUBWA WA WEMA
Juzi, Amani lilizungumza na shoga kipenzi wa Wema (jina lipo) ambapo alisema Wema amekuwa akimshangaa Zari kwa kumfuatafuata.
“Amesema wanawake waliotembea na Diamond ni wengi, kuna Wolper (Jacqueline), Aunt (Ezekiel), Penny (Peniel Mungilwa), Jokate (Mwegelo) na wengine. Yaani ni wengi sana, lakini yeye kila kukicha ana Wema tu.”
WASIWASI WA ZARI, UJAUZITO WA WEMA WATAJWA  
“Mimi nina wasiwasi kuna kitu zaidi kwenye moyo wa Zari. Anahisi katika wanawake wote, Diamond ana kila dalili ya kurudisha penzi kwa Wema ndiyo maana anamshambulia. Kwa nini asimshambulie Wolper au hao wengine?” alihoji shoga huyo na kuongeza kuwa chokochoko zimekuwa kubwa hasa baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa Wema kwa sasa ni mjamzito.
ZARI ANAMWAMINI WOLPER
Nyuma ya pazia kwa baadhi ya watu wa karibu na Zari, habari zinasema mrembo huyo yupo tayari amwone Diamond akiongea na Wolper popote hapa duniani na akalala usingizi mzito lakini siyo na Wema.
“Zari hamwamini Wema kwa Diamond hata chembe. Anatamani yeye akiwa Afrika Kusini ‘Sauz’ anakoishi au kwao Uganda, Diamond akaishi Msumbiji kwa muda hadi wakija wawe wote,” kilisema chanzo kimoja chenye ukaribu na Zari.
DIAMOND NI ‘PEACE TU’
Amani lilimsaka Diamond ili kumsikia anasemaje kuhusu malumbano yaliyopo kati ya mzazi mwenzake, Zari na zilipendwa wake, Wema ambapo alionekana kushangaa tu.
“Haa! Sasa ni nini kwani? Mbona peace (amani) tu. Mi naona kila mmoja yuko peace. Kwani kuna nini?” (simu ikakata).
WEMA MWENYEWE
Wema alipoulizwa, msimamo wake ni uleule, hawezi kujibizana na Zari. Alisema amelelewa kwa kufuata heshima, hivyo hawezi kujibizana na mtu aliyemzidi umri, akisema Zari ni kibibi.
NAYE WOLPER
Wolper ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na mwaka mpya, alipotafutwa na kuambiwa hayo, alicheka na kusema ni mambo ya kitoto kwake.
“Jamani! Hayo ni mambo ya kitoto tu. Watu waangalie mbele kwa sasa…teh! Teh! Teh!” alisema na kucheka Wolper.
HUKO NYUMA
Kabla ya sekeseke hilo ambalo kwa sasa ndiyo habari ya mjini, mara kadhaa Zari na Wema wamekuwa wakichonganishwa huku jina la Zari likitumiwa na timu yake kumdhalilisha Wema hasa juu ya kilio chake cha kukosa mtoto wakati mwenzake anao wanne.
chanzo GPL

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...