STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na 
kuwakandia mabwana aliowahi kutoka nao kimapenzi na kusema kuwa ni 
wababaishaji na sasa ni bora atafute mwanaume wa kumuoa.
Akipiga stori na Amani, Shamsa anayetikisa na Filamu ya Chausiku 
alisema, kwa sasa amejipanga kuolewa wakati wowote iwapo tu mwanaume 
mwenye sifa anazozitaka atajitokeza.
“Wengi niliowahi kuwa nao ni wababaishaji tu na wala sikuona mwanaume
 wa kuweza kunioa. Kwa sasa nimeshakua mtu mzima na ikitokea wa kunioa 
nipo tayari,” alisema Shamsa.
Awali Shamsa alikuwa akitoka na mtu aliyetambulika kama Dick na 
kupata naye mtoto mmoja, baada ya hapo ilidaiwa bidada huyo kaingia 
kwenye uhusiano na Nay wa Mitego.
No comments:
Post a Comment