Musa Mateja
 STAA
 kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Khadija Maige ‘Kadja 
Nito’,  hatimaye ameamua kufunguka na kusema kuwa, kwa maisha yake ya 
sasa ya kimuziki haoni kama kuna umuhimu wa kufikiria masuala ya 
kuolewa.
Akizungumza na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Kadja 
alisema kuwa, muziki sasa ndiyo kila kitu kwake hivyo hawezi kumpa 
nafasi mwanaume au kuzungumzia suala la ndoa hivi sasa.
“Naweza kuishi maisha yangu bila mwanaume, napata mshiko, nawasaidia 
ndugu zangu na mimi najimudu, mume wa nini maisha haya? Sasa ni muziki 
na mimi, mimi na muziki, mapenzi yasubiri,” alisema Kadja.
 
 
No comments:
Post a Comment