Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Zubeir Kabwe.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Zubeir Kabwe,
amevuliwa uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mwanasheria
Mkuu wa Chadema, ambaye pia alikuwa mmoja wa mawakili waliokuwa
wakikiwakilisha chama hicho katika kesi hiyo, Tundu Lissu.
Uamuzi huo umechukuliwa muda mfupi baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam, kutupilia mbali ombi lake la kuitaka kuizuia Kamati Kuu ya
Chadema kujadili kuhusu ubunge wake, hadi hapo rufaa aliyokuwa ameikata
katika Baraza Kuu itakapokuwa imesikilizwa.Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ambaye pia alikuwa mmoja wa mawakili waliokuwa wakikiwakilisha chama hicho katika kesi hiyo, Tundu Lissu ndiye aliyetoa tamko la kuvuliwa uanachama kwa Zitto.
“Katiba ya Chadema inasema wazi kuwa mwanachama yeyote atayekipeleka mahakamani, atakuwa amejiondoa uanachama wake endapo atashindwa kesi hiyo, hivyo natangaza rasmi kuwa Zitto Kabwe siyo tena mwanachama wa Chadema,” alisema Lissu.
Mgogoro kati ya Chadema na Zitto ulianza mwishoni mwa mwaka 2013 baada ya kugundulika kwa nyaraka zilizomhusisha Zitto na wanachama wengine wawili, Dr Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kwamba walikuwa na nia ya kufanya mapinduzi ya viongozi kwa njia zisizo halali.
Kufuatia jambo hilo, Chadema iliitisha kikao cha Kamati Kuu ili kuwajadili watu hao na kuchukua maamuzi, kilichofanyika Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe wake wote.
Wakati kikao hicho kikiendelea na kukiwa na dalili za Zitto na wenzake kutimuliwa, mbunge huyo kijana alikwenda Mahakama Kuu na kuweka zuio la kujadiliwa kwake na Kamati Kuu hadi rufaa yake katika Baraza Kuu la Chadema itakapokuwa imesikilizwa. Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilikaa Januari 2014.
Mahakama ilikubaliana na zuio hilo. Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa chini ya Jaji Richard Mziray huku Zitto akiwakilishwa na mwanasheria Albert Msando aliyekuwa akishindana na wanasheria watatu wa Chadema, Peter Kibatala, Tundu Lissu na John Mallya. Dr Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walifukuzwa uanachama na kikao kile cha Kamati Kuu.
Zitto mwenyewe alikuwa hajatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo ya chama chake, ambayo hata hivyo, ilitegemewa na wengi.
(HABARI: OJUKU ABRAHAM/GPL)
No comments:
Post a Comment