Tuesday, March 10, 2015

KAULI YA MAMA MARIA NYERERE BAADA YA KUZUSHIWA KIFO


Mama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jana jioni alizungumza na kituo cha runinga cha Taifa, TBC na kukanusha uvumi ulioenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameaga dunia.

Akizungumza na mtangazaji, Mama Nyerere alimuuliza, "ukiniangalia unanionaje?" ambapo mtangazaji alimjibu, "nakuona mzima!" huku wakitabasamu.

Mama Maria alisema huu ni mwaka wa uchauguzi, hivyo mambo haya ya uzushi si ya ajabu.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...