PEPO la ugomvi linazidi kumuandama staa wa Bongo Fleva, Khaleed
Mohamed ‘TID’, baada ya kusakwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumjeruhi
mtu mwishoni mwa wiki iliyopita, msanii huyo ametengeneza kicha cha
habari kwa mara nyingine akidaiwa kumpiga meneja wake aliyefahamika kwa
jina la Tall Mnyama.
Katika tukio la awali, TID alidaiwa kutembeza kichapo na kumjeruhi
James Richard, mkazi wa Jiji la Dar kwa kosa alilodai kuwa ni kupaki
gari kwenye eneo lake, maeneo ya nyumbani kwa msanii huyo,
Kinondoni-Sterio jijini Dar.
Tukio la kumpiga meneja wake, TID anadaiwa kulifanya katika Hotel ya
Element, Oysterbay ambapo inaelezwa kuwa msanii huyo alifika hotelini
hapo akiwa na wapambe wake na alipomkuta meneja huyo, alibishana naye
kwa muda mfupi kisha kumzaba kibao.
“Alimkuta mwenzake (Tall) kaka sehemu, akamsemesha na alipojibu tu
akamzaba kofi, lakini huyu meneja wake alikuwa mstaarabu, hakumlipizia.
Baada ya tukio hilo TID alitokomea na kama unavyojua sasa hivi anaishi
kama digidigi, mbaya zaidi watu wanasema asipompiga mtu hasikii raha,”
kilidai chanzo chetu.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, meneja huyo baada ya
kupokea kipigo hicho, alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi
Oysterbay kilicho chini ya Camillius Wambura (pichani) ambapo
lilifunguliwa jarada lililosomeka; OB/RB/3922/2015/TAARIFA.
Mwanahabari wetu alipomtafuta meneja huyo kuhusiana na tukio hilo,
alikiri kuwa limemtokea lakini akasema hakutaka kulivalia njuga lakini
alichokifanya ni kutoa taarifa polisi ili endapo atarudia, amchukulie
hatua kali zaidi za kisheria.
“Ni kweli TID alinishambulia kwa kunipiga kibao, iliniuma sana lakini
nimeamua kumsamehe, nilichokifanya ni kutoa taarifa polisi ili kama
atarudia nimfikishe katika vyombo husika,” alisema meneja huyo.
Jitihada za kumpata TID ili aweze kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa
matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.Jitihanada za kumpata
Wambura hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa siku
ya juzi.
No comments:
Post a Comment