Friday, March 6, 2015

HE...KICHAPO ALICHOPEWA NA WACHEZAJI YANGA, CHAMPA ULAJI NKONGO KIMATAIFA

Unaukumbuka mchezo huu? ilikuwa msimu wa 2012/13 Wachezaji walimshambulia mwamuzi Isreal Nkongo kwa maamuzi mabaya katika mchezo dhidi ya Azam, lakini sasa ni mtu wa kimataifa tu, pengine alijifunza mengi katika kisago hicho.
Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Israel Mjuni Nkongo amechaguliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) kati ya wenyeji Zesco FC ya Zambia dhidi ya AS Kaloum ya Guinea.
Katika mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa pili, Nkongo atasaidiwa na washika kibendera John Kanyenye na Josephat Bulali na mwamuzi wa akiba Waziri Sheha wote kutoka Tanzania, huku Kamisaa wa mchezo akiwa Mayixole Elvin Shishana kutoka nchini Afrika Kusini
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 13,14,15 Machi mwaka huu nchini Zambia.




No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...