Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inaendesha mafunzo kwa Maafisa Uandikishaji na Maafisa Waandikishaji Wasaidizi
kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mafunzo
yanafanyika katika Mikoa ya Lindi,Mtwara, Ruvuma na Njombe.
Mafunzo yalianza
kufanyika tarehe 2/2/2015 na yatamalizika tarehe 10/2/2015.
Mafunzo yalihusisha
matumizi ya Mashine za Biometric Voter Registration (BVR).
Mfumo wa BVR ndio
utakaotumika kuandikisha Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mmoja wa Maafisa wa Tume ya uchaguzi akiwa kwenye kituo cha kazi.
Baadhi ya Maafisa uandikishaji wakipatiwa mafunzo hayo.
Maafisa hao wakiapishwa kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment