Kocha Mkuu wa Yanga, Pluijm (wa kwanza kulia), haamini kile wachezaji wanachofanya siku ya mechi |
Kitendo cha timu
ya Yanga kuendelea kupata matokeo ambayo si mazuri kulinganisha na matarajio ya
wengi, kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm ameibuka na kusema kuwa
hajui tatizo liko wapi kwani kila mbinu anawafundisha na wanafanya vema
mazoezini lakini siku ya mechi wanacheza ndivyo sivyo.
Tofauti na
matarajio ya wengi ya kushuhudia mvua ya mabao kutokana na uwepo wake akiwa na
rekodi nzuri ya msimu uliopita ambacho kiliandikisha rekodi ya ushindi mkubwa
wa mabao 7-0 katika mechi mbili huku kikifunga mabao 19 katika mechi tatu
mfululizo; dhidi ya Komorozine, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons, lakini mambo
si mambo kwani msimu huu timu hiyo haijashinda zaidi ya mabao mawili.
Katika mechi
tatu zilizopita, Yanga imepata bao moja; dhidi ya Polisi Moro huku ikishikwa shati
uwanja wa taifa mbele ya Ruvu Shooting na Ndanda.
Akizungumzia
kikosi chake, Pluijm alisema, “Hata sielewi kabisa tatizo la kikosi changu liko
wapi, ninawapa kila mbinu lakini wawapo kwenye mechi sijui nini kinatokea,
lakini nadhani tatizo hili linatakiwa lkufanyiwa kazi zaidi ili kujiweka katika
nafasi nzuri ya kuwania ubingwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment