Saturday, February 28, 2015

NDOA YA TEMBA YAPUMULIA MASHINE

Mh. Temba.


NDOA ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ inadaiwa kupumulia mashine kutokana na madai ya kuwepo kwa usaliti baina yao.

Habari kutoka kwa chanzo kilicho karibu na wanandoa hao wanaoishi wilayani Temeke, kinasema kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya watu hao, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kusaliti, jambo linaloonyesha wakati wowote ndoa yao inaweza kusambaratika.
“Jamaa hayuko ‘peace’ kabisa na ndoa yake, yaani kila siku ni mgogoro, wife wake anamshutumu mshkaji kuwa msaliti kwa wanawake wengine na mke naye anatuhumiwa hivyohivyo ili mradi hakuna amani kabisa. Inaonekana kuna tatizo kubwa,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Gazeti la Risasi Jumamosi halikuweza kuwapata wanandoa hao kutokana na simu zao kutopatikana, lakini wakati linakwenda mitamboni, lilipata taarifa za kufikishwa mahakamani kwa Mheshimiwa Temba, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua, kitendo alichokifanya kwa Godfrey Deogratius anayemtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ akiwa na mke wake siku ya ndoa yao.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...