Aliyekuwa mke wa staa wa filamu nchini, Salim Mbegu ‘Slim’, Asia Morgan akiwa katika pozi.
“Mahakama hii imevunja baada ya mdai (mke) kusema hata iweje hawezi
kurudi tena kwa mumewe huyo kutokana na kuwa na wivu wa kupindukia na
kingine kibaya walivyokuwa kwenye mgogoro kuna mwanamke alikuwa
akijinadi kwa kupiga picha nyumbani kwa mumewe na kuzituma kwenye
mtandao wa kijamii wa Instagram,” alisema Hakimu Mwanaidi Madeni wa
mahakama hiyo.Hakimu aliamuru watalaka hao kugawana mali zote walizochuma pamoja likiwemo gari walilozawadiwa wakati wa harusi yao, ambalo ndilo lilikuwa chanzo cha mgogoro huo.Wakati mume akisema anaiheshimu hukumu hiyo ingawa anaona kama ni filamu, mke alionyesha furaha yake na kudai sasa ataishi kwa amani.
No comments:
Post a Comment