Mashabiki wa Ivory Coast |
Hatimaye kitendawili cha mbambe wa soka katika Bara la Afrika mwaka 2015, kimeteguliwa, baada ya Ivory Coast kutwaa taji hilo kwa mikwaju ya penalti 9-8 dhidi ya Ghana katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Bata, Guinea ya Ikweta.
Kipa wa Ghana Razack ndiye alitia 'nazi kwenye supu' baada ya kukosa penalti ya 9 iliyopanguliwa kiufundi na kipa wa Ivory Coast Aboubacar Barry 'Coppa' ambaye ndiye alimaliza kazi kwa kufunga penalti ya 9 na Ivory kubeba ndoo.
Mra ya mwisho Coast kulitwaa taji hilo ilikuwa miaka 23 iliyopita kwa kuibanjua Ghana mwaka 1992 huku Ghana wao wakiwa wamemaliza miaka 33 tangu walitwa.e
Kocha Herve Renard wa Ivory Coasta, ameandikisha rekodi ya kutwaa taji la Afrika akiwa na timu mbili tofauti, baada ya mwaka 2012 kulichukua akiwa na kikosi cha Zambia tena kwa kuitoa Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti.
Kabla ya fainali hii, timu hizo mara ya mwisho kukutana kwenye hatua kama hii, ilikuwa mwaka 1992 ambapo Ivory Coast ilitwaa ubingwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 11-10.
Rekodi ya kipekee ni kwamba, Ghana ndiyo timu pekee iliyokutana na Ivory Coast mara nyingi kuliko timu nyingine yoyote Afrika katika michuano hii. Zimekutana mara 9 na Ghana kushinda 5 na kutao sare moja na kufungwa 3.
Takwimu zinaonesha kuwa tangu mwaka 1965, timu hizo zimekutana mara 41 na Ghana inaongoza kwa ushinda, ikiwa imeondoka na pointi zote katika michezo 16, kufungwa mechi 15 na kutoa sare 10.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye michuano hii ilikuwa mwaka 2010 na Ghana kushinda kwa mabao 3-1. Kipigo kikubwa kuwahi kushuhudiwa kati ya timu hizi ni kile cha Ivory Coastal cha mabao 4 katika mechi tatu tofauti huku wao wakijivunia ushindi mkubwa kwa Ghana wa mabao matatu katika mechi tofauti.
Sare iliyokuwa na mabao mengi ni ya Februari 1882 ambapo timu hizo zilifungana mabao 5-5 katika michuano ya Mataifa ya Afrika Magharibi.
Kioja cha kipekee kilichijitokeza ni kitendo cha straika, Gervinho kutoangalia penalti hata moja baada ya kukaa akiangalia jukwaani akikwepesha macho wapigaji.
Staa na mkongwe, Didier Drogba licha ya kufanya kila kizuri kwenye soka, amestaafu bila kugusa kombe hilo, huku Yaya Toure akianza kazi ya unahodha kwa bahati ikiwa ni michuano yake ya kwanza na kutwaa ubingwa.
No comments:
Post a Comment