Mabingwa watetezi, Azam wameandikisha rekodi nyingine kwenye
ligi kuu, kwa kuwa timu ya kwanza kushinda mabao mengi msimu huu, baada ya juzi
Jumatano kuivurumisha Mtibwa Sugar mvua ya mabao 5-2.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi Complex,
mabao ya mabingwa hao yalifungwa na Kipre Tchetche na
Frank Domayo waliofunga mabao mawili kila mmoja pamoja na Didier Kavumba. Mabao ya Mtibwa yalifungwa na
Ame Ali na Musa Nampaka.
Kabla ya ushindi huo, Azam walikuwa wakishikiria rekodi ya
kutwaa ubingwa bila kufungwa pamoja na kucheza mechi 39 bila kufungwa kabla yakukutana na rungu la maafande wa JKT Ruvu ya Fred Minziro.
Ushindi wa juzi ulikuwa ni wa kwanza kwa wingi kwa Azam na ligi kwa
ujumla, ambapo kabla ya hapo timu iliyokuwa imefunga mabapo mengi ni Ndanda iliyopoichabanga Stand
United mabao 4-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi.
Rekodi nyingine mchezo huo ndio wa kwanza kushuhudiwa mabao
mengi- mabao saba na kufuta ile ya mabao matano ya Ndanda na Stand.
Msimu huu, Mtibwa ndio timu ilikuwa ikishikiria rekodi ya
kucheza mechi nyingi bila kupoteza, baada ya kushuka dimbani mara tisa kabla ya
kukumbana na ‘rungu’ la maafande wa Ruvu Shooting mapema mwezi uliopita.
Kichapo hicho kiliifanya kushindwa kupangua rekodi ya Hans
van Der Pluijm wa Yanga ya msimu uliopita ambapo alicheza mechi kama hiyo kabla
ya kusimamishwa na maafande wa Mgambo Shooting.
Abdallah Kibadeni Mputa anabaki na rekodi ya aina yake, baada
ya msimu uliopita kuiongoza Simba kucheza mechi 10 bila kufungwa, lakini
‘utemi’ wake ulisimama kwa Azam katika mechi ya 11.
No comments:
Post a Comment