Tuesday, February 24, 2015

BARCA YAINYOA MAN CITY UEFA, JUVE YAWAFUNGA MIDOMO WAJERUMANI

Kiulainiiiiii...Suarez akumbushia mavituzi yake enzi akiwa na Liver, awalaza na mawazo Man City. Kulia picha ya chini Messi akificha uso baada ya penalti yake kupanguliwa.
 Wazee kwa 'tik-taka game', Barcelona wamezidi kudhihirisha ubora wao, baada ya kuifumua Manchester City tena nyumbani kwake, Etihad kwa jumla ya mabao 2-1, idadi sawa na kicheko cha KIbibi Kizee cha Turin, Juventus waliowafundisha soka Wajerumani wa Borussia Dortmund katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’.
Luis Suarez ndiye aliibeba Barca katika mchezo wa leo, kwa kufunga mabao yote, kwa kujitengenezea mwenyewe moja na nyingi akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na staa, Lionel Messi, yote akiyafunga kipindi cha kwanza.
Vijana wa Man City walionekana kuzidiwa soka kipindi cha kwanza, huku pengo la Yaya Toure likionekana wazi ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, hata hivyo walibadilika kipindi cha pili hasa baada ya kuigia kwa Fenandinho aliyechukua nafasi ya Samri Nasri.
Mabadiliko hayo yliipa nguvu City na kuanza kulisakama lango la Barca, tofauti na kipindi cha kwanza na kufuanikiwa kupata bao kupitia kwa Sergio Aguero.
Messi aliinyima bao la usiku timu yake, baada ya mkwaju wake wa penalti dakika ya mwisho kabisa, kupanguliwa na kipa wa Man City, Joel Hart kabla ya Messi kuunganisha tena mpira kwa kichwa, lakini ukatoka nje.
Kichapo hicho kinaiweka pabaya Ciy kwani inahitaji ushindi wa lazima ugenini katika mchezo wa marejeano kule Nou Camp, lakini habari mbaya ni kumkosa beki wa kushoto, Gael Clichy aliyepigwa kadi nyekundu katika mchezo wa leo, lakini Toure atakuwa anamaliza adhabu yake.

Juve vs Dortmund

Mabao ya Carlos Tevez na Alvaro Morata yaliipa ushindi wa mabao 2-1 Juve mbele ya Dortmund , mchezo uliopigwa Turin, Italia. Mchezo huu ni wa kwanza kwa timu hizo kukutana tangu mwaka 1997, ambapo zilikutana fainali na Dortmund kushinda kwa 3-1 na kuivua ubingwa Juve, lakini leo wamelipiza kisasi hicho.
El Apache..!!! Straika tegemeo wa Juve, Carlos Tevez a.k.a El Apache, kushoto mbele, akikwamisha mpira langoni mwa Dortmund katika michuano ya Uefa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...