Sunday, June 29, 2014

WASHIRIKI 20 WA SHINDANO LA TMT WAINGIA RASMI KAMBINI JANA USIKU, TAYARI KWA SAFARI YA KUWANIA MILIONI 50‏



Muonekano wa TMT House ambayo washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents wameweka kambi rasmi kuanzia jana Usiku kwa mchakato wa kuwania Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane.


Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la TMT wakiingia kambini hapo jana usiku.

Mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kusini, Mwanaafa Mwizago akiingia rasmi kambini hapo jana wakati wakitokea kwenye matembezi. Washiriki wote 20 ambao ni washindi kutoka Kanda sita za Tanzania sasa wapo kambini kwaajili ya kujifua ili kuwania kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.

Washiriki wakiwa ndani ya Nyumba ya TMT tayari kwa kambi.

Washiriki wakipewa maelekezo mara baada ya kuwasili kambini hapo jana.


Na Josephat Lukaza - Proin Promotions - Dar Es Salaam.
Washiriki 20 kutoka Kanda sita za Tanzania wameingia rasmi kambini hapo Jana mara baada ya kumaliza zoezi la Kupima Afya, kutembezwa sehemu mbalimbali za Jiji la Dar pamoja na Ofisi za Global Publishers.

Washiriki hao watakaa kambini kwa Siku 64 ambapo wataanza rasmi kufundishwa Hapo kesho siku ya Jumatatu na walimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo ambapo baadae sasa baadae zoezi la kuanza kuwapigia kura washiriki hao litaanza na hatimaye watanzania ndio watakuwa majaji kwa washiriki hao ambapo mshindi mmoja wa Shilingi Milioni 50 atapatikana katika Fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Zoezi la Upigaji kura litaanza mapema wiki ijayo ambapo washiriki wote watakuwa tayari washapewa namba za ushiriki na hatimaye watanzania kuweza kuwachagua washiriki wanaowaona wana vipaji.
Zoezi hili la kupiga kura litapelekea Washiriki wawili kuondolewa kila wiki katika Kambi ya TMT ambapo pona yao ni kutoka kwa Watanzania ambao ndio watakuwa majaji kwa kuwapigia kura.

Vilevile Mara baada ya washindi hawa wa kanda kuingia kambini Vipindi vyetu vitaendelea Kurushwa kila siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku na Kurudiwa kila Siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa tano usiku kupitia Runinga ya ITV.
Tunawaomba watanzania kuendelea kutizama vipindi vyetu kwani vimekuwa na mvuto wa hali ya juu sana lakini pia kuendelea kuwawezesha

Washiriki wanaowaona wana vipaji ili kuwa ushindi.


Namba za washiriki zitaanza kuonekana katika Kipindi chetu kijacho ambapo Sasa watanzania wataanza kuwapigia kura kwenda namba 15678

Na ili kuweza Kufahamu taarifa zaidi za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...