Friday, May 9, 2014

RAY C ASIMULIA ALIVYOKICHUNGULIA KIFO

Stori: MUSA MATEJA
MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.

Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akiwa kwenye red carpet ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards.

Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.

Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.

Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.


“Huwezi kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue, walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu.

“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.

“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.

“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo. “Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!”
alimalizia Ray C.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...