Saturday, January 25, 2014

MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE RAMADHANI BWANAMDOGO WAZIKWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa Chalinze,Mh. Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Miono Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani leo.


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe (CHADEMA) wakati wa mazishi ya mbunge wa Chalinze Marehemu Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika huko Miono Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani leo.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono. Picha na OMR.

 

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...