Tuesday, January 21, 2014

FLAVIANA MATATA FOUNDATION AENDELEA KUKUZA ELIMU NA PSPF



Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo,wakati akizungumzia mradi wake unaotambulika kama “FMF Stationeries Project”; mradi unaojihusisha na uhamasishaji wa mashirika mbalimbali, taasisi za serikali na watu binafsi kuchangia na kusambaza vifaa mbali mbali vya shule kama vile madaftari ya mazoezi, kalamu za wino, kalamu za risasi, rula, mikebe, vifutio na mabegi ya wanafunzi, kwa wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu hapa nchini Tanzania.

Afisa Mawasiliano,Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Hawa Kikeke (kushoto) akizungumza na akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na jinsi Mfuko huo ulivyoweza kushirikiana na Flaviana Matata Foundation katika kusaidia kuinua elimu hapa nchini,ambapo kwa ushirikiano huo wamefanikiwa kusambaza vifaa vya shule (stationery kits) vinavyojumuisha mabegi ya shule, madaftari ya mazoezi na vitu vingine,Katika awamu ya kwanza ya mradi (Januari 2014) PSPF wamechangia “FMF Stationery kits” 1000 kwa wanafunzi wasiojiweza mkoani Pwani.

Mratibu wa Flaviana Matata Foundation (FMF),Lusajo Mwaisaka akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Mpango Mkakati wa Flaviana Matata Foundation kuendelea kusaidia wanafunzi wasiojiweza katika maeneo mbali mbali hapa nchini.Kushoto ni Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata.

Muanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF),ambaye ni Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata pamoja na Afisa Mawasiliano,Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Hawa Kikeke wakifurahia jambo wakati wa kupata picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...