Wednesday, November 27, 2013

MAITI HUFUKULIWA MAKABURINI ILI KUBADILISHWA NGUO HUKO INDONESIA


Pichani ni baadhi ya wafu waliofukuliwa kaburini na kuvishwa nguo Indonesia.

KILA mwaka huko Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila za ajabu kuhusu vifo na maisha yanayofuata baada ya mtu kufa.
Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.
Torajan huishi katika maeneo ya milimani na hawataki kujulikana sana katika jamii, japokuwa wana mila na desturi zao zilizoenea katika jimbo la Sulawesi.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...