Thursday, November 28, 2013

AIRTEL YAWANOA WATANGAZAJI WA RADIO MBALIMBALI LEO


Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akisistiza jambo kwa watangazaji wa vipindi vya redio mbalimbali (hawapo pichani) kuhusu vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni bingwa" itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.Kulia kwake ni ofisa wa matangazo wa Airtel Bw. Abdallah Gunda.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kujiunga na promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni Bingwa" itakayowawezesha wateja wa Airtel kushinda tiketi 2 za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za Manchester United kila wiki au mamilioni ya pesa kila siku. Kutoka kulia ni Meneja masoko wa Airtel Upendo Mkini akifuatiwa na meneja msimamimizi wa promosheni hiyo Fatma Ngororo.
Toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airte Tanzania Bw Jackson Mmbando akibadilishana mawazo na watangazaji wa kipindi cha jahazi bw Musa Huseni (kati) na Ephraem Kibonde mara baada ya mkutano maalum na watayarishaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio kwa lengo la kuwaeleza vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel Mimi ni bingwa" inayowawezesha wateja wa Airtel kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...