Monday, October 7, 2013

SERENGETI FIESTA ILIVYOFANA MOSHI



Msanii mkongwe katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes akiwaimbisha mashabiki wake kibao waliofurika vilivyo ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi ambapo tamasha la Serengeti fiesta linafanyika.

Kundi la Weusi likiongozwa na Joe Makini wakilishambulia jukwaa usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta uwanja wa Majengo mjini Moshi.

Mashabiki na ushabiki wao live.

Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,Menina akiimba kwa hisia jukwaani

Mkali mwingine wa bongofleva anaefanya vyema kwenye muziki huo,akitambulika kwa jina la kisanii Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye wakati wa tamasha la serengeti fiesta likiendelea kwenye uwanja wa Majengo,mjini Moshi.

Mwanadada Linah akimpagawisha shabiki wake vilivyo jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.

Mkali wa shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Nigeria Jay Martins akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa Moshi waliofika kwenye tamasha la fiesta ndani ya uwanja wa Majengo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye amekuwa akifanya vyema tangu aibuliwe na Serengeti supa Nyoya kutoka jijini Mbeya,Neylee kwa sasa anakula matunda ya ufanisi wake wa kisanii katika anga ya muziki huo,pichani akiwa kwenye jukwaa la serengeti fiesta usiku huu mjini Moshi kwenye uwanja wa Majengo ambapo tamasha hilo likiendelea.

Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka nyumba ya vipaji THT,Ally Nipishe akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta usiku huu.

Mzee wa masauti kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Acudo,Christian Bella akiimba jukwaani.


Sehemu ya umati wa watu kutoka mjini Moshi wakiwa kwenye tamasha la fiesta usiku ndani ya uwnaja wa Majnego.

Mwanamuziki wa bongofleva kutoka THT,pichani kati Linah akicheza kwa madaha kabisa na madansa wake jukwaani usiku huu.

Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,aitwaye Menina akiimba jukwaani na madansa wake.

Wasanii wanaounda kundi la Jambo Skwadi wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee kabisa usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.

Wakazi wa mji wa Moshi wakishangweka
Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Nigeria Jay Martins akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa Moshi waliofika kwenye tamasha la fiesta ndani ya uwanja wa Majengo.

Msanii wa Bongofleva,atambulikae kwa jina la kisanii AY,akiwaimbisha wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,lilofanyika ndani ya uwanja wa Majengo,ambapo pia mwanamuziki maarufu kutoka nchini Nigeria Jay Martins alitumbuiza pia.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...