MAKAMUZI YA BENDI YA TWANGA PEPETA NEW MAISHA CLUB
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akionyesha uwezo wake wa kudansi ndani ya ukumbi wa New Maisha Club.
Wanenguaji wa kike wa bendi ya Twanga Pepeta wakipagawisha mashabaki jukwaani.
BENDI ya muziki wa dansi nchini ya African Stars ‘Twanga Pepeta
International’, usiku wa kuamkia leo wamewapagawisha mashabiki wake
baada ya kutoa burudani ya nguvu ndani ya ukumbi wa New Maisha Club
uliopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta wakitoa burudani ya kutosha kwa mashabiki waliokuwa ndani ya ukumbi huo.
Mmoja wa wanenguaji Samilah Shaban (kushoto), akimnong’oneza jambo rafiki yake.
Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka akifuatilia kwa makini burudani ukumbini hapo.
Wanenguaji wa kiume wa wa bendi ya Twanga Pepeta wakidansi jukwaani ili kukonga nyoyo za mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment