Naibu waziri wa Nishati na Madini Mh.Steven
Masele akiongea jambo katika Semina ya Kamata Fursa Twenzetu iliyofanyika
mapema leo ndani ya Ukumbi wa Shinyanga Vijana Centre mjini hapo.
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini Mh.Steven
Masele leo ametumia muda wake kwa wakazi wa Shinyanga katika kuwaelimisha na
kuwaonyesha namna ya kutumia Fursa mbalimbali zilizopo mjini hapo.
Akizungumza katika Semina ya Serengeti Kamata
Fursa Twenzetu ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Centre aliwataka vijana na
wakazi wote wa mji huo kujiweka sawa mara viwanda mbalimbali vya kusindika
Pamba na kutengeneza nguo vitakapoaanza waweze kutumia fursa katika nafasi
muhimu za kazi na ujasiliamali mbalimbali utakaokuwepo.
Mkurugenzi wa Vipindi na Maendeleo wa Clouds
Media Group Ruge Mtahaba, akiwafundisha wakazi wa Shinyanga namna ya kutumia
Fursa kupitia rasilimali mbalimbali zilizopo mjini hapo katika kujikwamua
kimaisha.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Maxcom Africa
Bernard Munubi akiongea jambo kwenye semina hiyo.
Watangazaji wa Clpuds FM, Millard Ayo (kushoto),
na Shafi Dauda wakichangia jambo katika kuwaonyesha fursa wakazi wa Shinyanga.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya TPSF, Jane
Gonsalves (kulia),akimuuliza swali mmoja wa wadau waliohudhulia kwenye Semina
ya Kamata Fursa Twenzetu ndani ya Ukumbi wa Shinyanga Vijana Centre mapema leo.
Adam Mchomvu naye hakuwa nyuma kuwaonyesha namna
ya kutumia fursa kupitia katika utangazaji.
No comments:
Post a Comment