Msanii wa kughani mashairi
Mrisho Mpoto, akizungumza na wakazi wa Iringa waliyojitokeza kusikiliza mafunzo
ya namna ya kujikwamua kimaisha kwa kutumia Fursa ya rasilimali zilizopo mjini
Iringa.
SEMINA ya Serengeti Fiesta Kamata Fursa 2013,
mapema leo imeendelea ndani ya Ukumbi wa ST.Dominic mjini Iringa, ambapo watu
mbalimbali wamepata fursa ya kujua namna ya kutumia rasilimali zilizopo mkoani
hapo kwaajili ya kujikwamua kimaisha.
Mfanya biashara mkubwa wa mjini Iringa Salim
Asas (kushoto),akionyesha baadhi ya Fursa zilizopo Iringa kwa kuonyesha
kitunguu cheupe kama moja ya bidhaa za thamani zilizopo mjini hapo na kulia, ni
Mtangazaji wa Clouds FM Wasiwasi Mwabulambo akichukua kitunguu hicho kwaajili
ya kukionyesha.
Salim Asas akiongea na baadhi ya wakazi wa
Iringa waliyojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa Twenzetu.
Mdau mkubwa wa Michezo nchini David Mwakalebela
naye alipata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa Iringa na kutoa kiasi cha
shilingi milioni moja kwaajili ya kuwawezesha wakazi wa mkoa huo watakoweza
kutumia fursa ya rasilimali zilizopo mkoani hapo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi
Kipya Bongo,Nick wa pili akiwaonyesha wakazi wa Iringa namna ya kutumia fursa
zilizopo mkoani hapo kwaajiri ya kujikwamua kimaisha.
Watangazaji wa Cluds FM, DJ Fetty (kulia), na
Anord Kayanda wakifatilia kwa makini semina hiyo.
Mwakilishi kutoka NSSF Makao Makuu Salim
Halfani, akizungumzia Fursa kwa upande wa NSSF wanavyoweza kuitumia fursa
wakazi wa Iringa katika kupata mikopo itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.
Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo akionyesha moja ya tisheti yenye jina lake aliyotengenezewa na mbunifu wa mavazi wa Iringa kama moja ya Fursa yake aliyoitambua mjini hapo na kutumia kwa kumpatia mtangazi huyo
Mtu wa nguvu Millard Ayo (kulia), akiwa kwenye pozi na Dreva Philimon muda mfupi baada ya kumaliziki kwa semina ya Kamata Fursa Twenzetu ndani ya Ukumbi wa ST. Dominic mjini Iringa.
No comments:
Post a Comment