Monday, September 2, 2013

MISS TANZANIA 2012 BRGITTE AAHIDI KURUDI NA TAJI LA MISS WORLD 2013 LITAKALOFANYIKA NCHINI INDONESIA


Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lymo, ameondoka nchini leo kwenda nchini Indosia katika kambi ya Miss World 2013. Pichani juu kushoto ni Brigitte akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii  na Mkurugenzi wa mashindano hayo Hasheem Lundenga wakiagana tayari kwa safari hiyo. 

AKIZUNGUMZA  na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka nchini akiwa uwanjani hapo Brigitte ameahidi kufanya vyema katika mashindano hayo huku akiwaomba watanzania kumpa suport kwa kumpigia kura pindi zoezi hilo liytakapo anza kupitia tovuti ya Miss World.

Lundenga akizungumza huku Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfed na mama yake wakisikiliza.

Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.
 



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...