Friday, June 7, 2013Spika Makinda awatolewa uvivu wabunge wapenda vijembe

Spika wa Bunge Anne Makinda juzi alikemea tabia ya baadhi ya wabunge na Mawaziri kutumia dakika zao vibaya badala ya kuchangia hotuba wanatumia muda huo kuwashambulia wenzao.

Makinda alitoa kauli hiyo juzi wakati akiahirisha kikao jioni muda mfupi baada ya Bunge kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Katika hotuba hiyo, wabunge wa upinzani walikuwa wakielekeza michango yao kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa wakimtaka ajiuzulu.

Makinda alisema kuwa tabia hiyo ni kero kubwa kiasi cha kufanya wananchi waone kuwa Bunge ni sehemu ya malumbano na vijembe. Hii sio mara ya kwanza kwa Spika Makinda kuonya tabia hizo za wabunge.

kwani alishawahi kuonya na kuwakataza wabunge pia kutumia muda mwingi kuzungumza na Waziri Mkuu anapokuwa katika kiti chake ndani ya Bunge.

“Tabia hiyo ni mbaya tena inavunja heshima ya Bunge, nilishawaambia mara zote kuwa hapa Watanzania wanatuona kwa kila tunalolifanya humu ndani, acheni kabisa tabia hiyo kuanzia sasa,” alisema Makinda.

Alisema kuwa tabia za wabunge kulumbana ndani ya Bunge na kunyoosheana vidole imekuwa ni kero kiasi cha kuvunja kanuni za Bunge ambalo haliruhusu vitendo hivyo.

Aliwataka wabunge kurejea katika Kanuni za Bunge ambazo zinazuia mtu kunyooshewa na kutajwa moja kwa moja na badala yake wabunge wanatakiwa kuzungumza na kiti cha Spika.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...