Thursday, June 6, 2013

Hatimaye: Mangweir apumzishwa kwenye makazi yake ya milele
Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri. Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye Instagram.

Naye Lady Jaydee kupitia Twitter ameandika: Mpk hapa tulipomsindikiza panatosha. Mungu amrehemu, kazi tumeimaliza. Life goes on.”


Hapa ndipo alipolala Mangweir.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...