Wednesday, May 15, 2013

SWAHILIFILMS WAZINDUA RASMI KAMPENI ZA KUTUNISHA MFUKO WAKE.




Mwenyekiti Ngabwe akipeana mkono na Mh. Joel Bendera MorogoroKATIKA kuhakikisha kuwa wasanii wanajenga misingi ya kuwa na uwezo wa kujitegemea na kuzalisha Sinema bila kusubiri msaada kutoka serikalini na taasisi nyingine Swahilifilms wamefungua mfuko, Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Joel Bendera amezindua rasmi kampeni za uchangiaji katika kuutunisha mfuko wa swahilifilms ofisini kwake siku ya Ijumaa.

Mkuu wa mkoa huyo pia alizindua rasmi kauli mbiu ya Swahilifilms ijulikanayo kama ‘Weledi, Maadili na Uchumi imara’.
Kampeni hizo zinaendelea kwa wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na tasnia ya filamu Tanzania, katibu bwana Ignas Mkindi amesisitiza umoja kwa taasisi zinazotaka kuleta mapinduzi ya kimaendeleo katika tasnia ya filamu Swahiliwood, pia kujikita katika kufanya kazi zenye Weledi lengo ikiwa ni kufikia soko la kimataifa ambalo bado linasuasua.

Mh. Joel Bendera akiongea na Moses Mwanyilu wa Steps Enter.


Wadau wa Swahilifilms katika picha ya pamoja na Mkuu wa Morogoro Mh. Joel Bendera.Katika uzinduzi huo, mkuu wa mkoa alikabidhiwa rasmi kadi maalum na mwenyekiti wa swahilifilms, Sosteness Ndassi maarufu kama Ngabwe kisha mkuu wa mkoa huyo akawakabidhi wawakilishi wa taasisi na makampuni yaliyoichangia swahilifilms kabla ya uzinduzi huo.


Ngabwe akipeana na mkono na Mh. Bendera.Baadhi ya taasisi na makampuni yaliyokabidhiwa kadi hizo ni Bodi ya Filamu Tanzania, makampuni ya Steps Entertainments na Splash pamoja na diwani wa kata ya Uwanja wa Taifa, Morogoro mheshimiwa Zumo Makame.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...