Ruge Mutahaba.
Akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast leo, Mkurugenzi waClouds Media Group, Ruge Mutahaba ameelezea kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na msanii Judith Wambura 'Lady Jaydee' wiki iliyopita. Ruge amesema vita ya Lady Jaydee ameielekeza sehemu isiyo sahihi, kama tatizo ni Bendi ya SkyLight basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine pia amesema hiyo bendi sio ya kwake kama anavyodhani ila ni ya aliyekuwa mfanyakazi wa Clouds Sebastian Maganga kama alivyokuwa yy hivyo hawana budi kumsapot. Ameelezea Clouds ilipomtoa Jaydee mpaka sasa alipo tena akawaasa wasanii kukubali kupokezana vijiti na kujiandaa kwa maisha yajayo na kusema tuhuma za Jide haoni kama zina mantiki kwaniClouds ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria na kuthibitisha kauli yake hiyo boss Ruge ameamuru leo katika stesheni hivyo kutokupiga nyimbo za bongo flava. Ruge alienda mbele zaidi kwa kusema siyo vizuri watu kuchafuana katika mitandao ya kijamii, kama kuna tatizo ni vyema kama Jide ana hoja za msingi atafute watu wenye hekima yuko tayari kukaa chini na kuzungamzia hili suala, Ruge amemalizia kwa kusema ifike kipindi wasanii wakabaliane na changamoto na sio kuziona ni tatizo
No comments:
Post a Comment